FT: Portugal 0-1 Spain | World Cup 2026 | AT&T Stadium | 6 Julai, 2026 | 4:00 Usiku | Portugal yaaga mashindano

FT: Portugal 0-1 Spain | World Cup 2026 | AT&T Stadium | 6 Julai, 2026 | 4:00 Usiku | Portugal yaaga mashindano

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Leo ni fire tu! Bonge moja ya mechi CR7 anakumbukumbu nzuri alicheza na Spain alifunga magoli 3 katika mechi nzito sana kuwahi kutokea world cup 2018 kule Urusi
#####
Majirani Ureno na Hispania watakutana jijini Arlington katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026, ukiwa ni mkutano wao wa kwanza tangu fainali ya UEFA Nations League mwaka jana.

Ureno ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia katika hatua ya 32 bora kwa taabu, huku bao la ushindi likifungwa mwishoni mwa mchezo. Ingawa haikuwa rahisi, jambo muhimu kwao lilikuwa kufuzu, huku sasa wakisaka kufika robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Kwa upande wa Hispania, walionyesha ubora mkubwa kwa kuichapa Austria mabao 3-0 na kufuzu hatua ya 16 bora. Ushindi huo uliifanya Hispania kuwa timu ya kwanza tangu Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia 2014 kutoruhusu mpinzani kupiga hata shuti moja lililolenga lango katika mchezo wa hatua za mtoano wa Kombe la Dunia.
 
Hispania pamoja na kuwa na wachezaji wazuri kocja wake ameshindwa kutengeneza mfumo wa kuwaunganisha pamoja wakitolewa sitashangaa.
 
Back
Top Bottom