Execute
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 3,000
- 7,336
Ni siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu sana na mashabiki hapa Tanzania, kule Angola na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Mnyama mkali anashuka dimbani akiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao matatu kwa moja ugenini.
Anaenda kumaliza ngwe na kuingia hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Tutakuwa hapa tukipeana taarifa mubashara. Mechi itaanza saa kumi kamili Alasiri.
Kikosi cha mnyama mkali
=======
01' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo dimba la Benjamin Mkapa.
03' Moses Phiri anafika lango la De Agosto lakini anadondoka mwenyewe.
07' Simba wanacheza pasi fupi nyingi ndani ya nusu yake.
12' Simba wapata kona ya kwanza ya mchezo, kichwa cha Inonga kinapaa juu ya goli.
13' 🟡Many Rashid wa De Agosto analamba kadi ya kwanza ya njano baada ya kumdondosha Okra akielekea langoni.
20' Mpira uko chini zikiwa ni pasi maridadi kutoka kwa timu zote mbili.
21' Simba wanapata kona ya pili ambayo inashindwa kuleta mabadiliko kwenye ubao.
25' Sakho anapunguza watu na kuingia mwenyewe, beki wa De Agusto anapangua mipango.
30' Phiri na Okrah wanajaribu langoni mwa De Agusto, gonga yao inazaa kona ya tatu kwa Simba bila ya matokeo.
32' 🟡 Kadi ya njano kwa Venancio baada ya kumvuta shati Chama.
33' ⚽Moses Phiri anaiandikia Simba bao la kwanza, pasi safi kutoka kwa Zimbwe Junior aliepokea mpira kutoka katikati ya uwanja.
43' Onyango anauza mpira, free kick kuelekea Simba. Free kick ya De Agosto inagonga ukuta.
45+2' Mpira mapumziko.
=====
50' Okra anajaribu kuwapita walinzi wa De Agosto lakini anapiga njeeeeee.
51' Venancio anapewa onyo kali baada ya kumzuia Kanoute kwenye njia, Venancio tayari ana kadi ya njano.
58' Simba wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa katikati ya dimba huku wakijaribu kufika kwenye lango la De Agosto mara chahce.
59' Faulo ya tisa kwa De Agosto, Mzamiru yuko chini.
63' Simba inapoteza mpira baada ya kujaribu kona fupi, mpira wa kurusha kuelekea Simba.
64' Chama anafanya udambwi na kumpita mlinda Mlango wa De Agosto, pasi inashindwa kimfikia Moses Phiri.
65' Phiri anapata nafasi nyingine na kuachia mkwaju mkali, kipa anapangua. Kona.
68' 🔁 Kibu Deniss anaingia kuchukua nafasi ya Sakho.
72' 🟡 Antonia Silva anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Okra.
77' 🔁Habib Kyombo anaingia kuchukua nafasi ya Okrah aliyeumia.
78' 🔁 Zimbwe JR nae anaenda bench na nafasi yake inachukuliwa na Gadiel Michael Mbaga.
87' Gadiel anapewa kadi ya njano baada ya kuvuta bukta ya mchezaji De Agusto.
89' Manula anaingia mwenyewe mpaka katikati ya uwanja.
90' Dakika tatu zinaongezwa kuhitimisha mpambano.
90+1' Nyoni na Mkude wanaingia, Israel Mwenda anaenda bench.
90+3' Mpira unatamatika dimba la Benjamin Mkapa na Simba wanasonga mbele kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya De Agosto.