FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

Mechi ya leo imeamulia na saikolojia ya wachezaji, nyuso za wachezaji wa Simba walikuwa na shauku kubwa sana ya kudhihirisha kitu mbele ya wapenzi wa mpira wa miguu ulimwenguni kutokana na kukosolewa kwao kuwa ni kikosi kibovu huku Yanga kwavile wanaongoza ligi na hawajapoteza moja tu wakiaminika kuwa ni bora zaidi. Hali ya kujiamini na kuchukulia mazoea ikaingia kwa mashabiki, wachezaji hadi benchi la ufundi.

Simba walijiandaa sana kiakili kwa hali ya juu hivyo ikawa ni rahisi kwa kuwa ndani ya mchezo katika game plan yao. Yanga kipindi chote cha kwanza walipoteana kabisa, akili zao zilikuwa hazijatulia, halafu wakawa wana mambo mengi mno uwanjani wakati wachezaji wa Simba walikuwa ni kwenda direct na kwa haraka golini kwa Yanga. Kutokana na kuwa na utulivu makosa kwa wacheza wa Simba yakawa ni machache kulinganisha na Yanga waliopotea mchezoni. Kilichowakuta leo ni kama surprise, na yote hiyo ni kutokana na kutokuheshimu mpinzani wako.

Kama hii mentality itabadilika, basi kule kwa Rivers Yanga itapigwa goli nyingi sana. Maana saivi kila mtu anamuonea Simba huruma huku wakijiona wao wapo semi, ila mambo yanaweza kwenda tofauti.

Mwisho namalizia kwa kusema, Yanga msimu ujao ubingwa wa NBC mnapaswa mjipange sana. Ukiangalia kikosi cha Simba kinahitaji tu kiungo mkabaji basi. Ila Yanga inahtaji wapishi wa magoli haswa na namba tisa ambaye asubiri nafasi kumi ndio apate goli moja.
Pia soma hapa namna nilivyompa tahadhari mwana yanga mwenzangu kuamini Simba ni mbovu.

TATIZO LA KUNUNUA MAREFA HILO
 
Mgema akisifiwa [emoji23]
IMG_20230416_193008.jpg
 
Back
Top Bottom