Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Kumbe vifuani mwenu mmehifadhi maumivu makubwa na hamsemi?Nilichokuwa nakitaka ndio hiki kimetokea leo.
Ishu haikuwa sio tu kumfunga Yanga
Bali ni kumfunga Yanga akiwa full compact plus na vile virutubisho vyake vya jezi nyeusi kuihusisha na bahati.
Mwaka jana niliposikia taarifa kuwa Mayele anataka kuuzwa mpaka Senzo kutishia kuondoka endapo atauzwa, nilikuwa mtu niliye tofautiana mtizamo na baadhi ya mashabiki wenzangu wa Simba.
Mimi sikutaka hilo litokee, hiyo yote ilikuwa kwa ajili ya siku kama ya leo.
Tungewafunga wakiwa wamepungukiwa na wale wachezaji wao nyota ningefurahi kama ushindi kumfunga mtani ila vibe lingekuwa too low.
Kwasababu kile kipindi tuwafunge bao 4-1 ni ukweli usiopingika kuwa hawakuwa na kikosi bora. That's why unaona hata wao utetezi wao ulikuwa "tulikuwa tuna kikosi kibovu"
Leo kila waliyetaka kumuona uwanjani, alikuwepo.
Kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji wote leo walikuwepo, hakukuwa na majeruhi, hakukuwa na wachezaji waliokosa mechi sababu ya kadi za njano.
Leo labda watafute lawama kwa kumkosa Feisali. (Kitu ambacho nitawaona vigeugeu kwasababu wao ndio waliosema no Feisali no problem)
Mwisho nasema mjifunze kuiheshimu Simba, muache ushamba wa kuamini rangi ya jezi kuwa ndio yenye bahati.
Mechi yenu inayofata aanzeni upya hesabu zenu, kuanzia ule ukiritimba wa kufurahia kila mechi kufunga goli hadi unbeaten
Sikujuwa kama ulikuwa unaumia kiasi hiki.
Hii ni ushahidi tosha ya Watanzania walivyo huko mitaani watu wanaumia na mafanikio yako lakini hujui tu.