Iamwhoiamm
JF-Expert Member
- Oct 18, 2022
- 503
- 887
Nimeliona hilo shuti ...hili shuti lingepigwa upande wa pili wa nchi wangelisifia mwaka mzima ila sisi walaaaaSakho Goooooooooooooaaal gooal
Pape Sakho anaandika bao la kwanza kwa shuti kali la umbali, na kumuacha golikipa Ssituba akiruka bila mafaniko.
Simba SC 1-0 Ihefu FC
Nilikuwa napiga stori na shabiki mmoja wa Simba anasema hii timu Mungda imemshindaKama kweli unatazama mechi za Simba vizuri kabisa na unaujua mpira sidhani kama utamlaumu kocha, kazi yake anaifanya vizuri kwa 100%. Changamoto pale ni eneo la mwisho kwenye ufungaji hakuna utulivu na wote wanaopewa nafasi ya kucheza pale mbele hawajafit kabisa. Ukitaka kumlaumu Mgunda jiulize kwanza timu aliikuta katika hali gani na je wale wachezaji yeye ndio alipendekeza wasajiliwe?!!
Hata ukirejea kutazama baadh ya mechi mfano vs Yanga, Azam, hao Singida na hata Mtibwa pamoja na kuwa walifungwa goli 5 lakini nafasi nyingi za kufunga magoli zilitengenezwa kwenye mechi zote hizo lakini washambulizi wanakosa umakini kabisa.. hii sio shida ya Mgunda amemuamini na kumpa nafasi kila mchezaji pale.. Wakati wake wa kulaumiwa apewe timu asajili silaha zake za maangamizi ashindwe ndio tuje kumlaumu hapa..Nilikuwa napiga stori na shabiki mmoja wa Simba anasema hii timu Mungda imemshinda
Hapo ni baada ya kupata sare na Singida
Nikamuambia nipe sababu, akasema kwanza jinsi anavyomuona tu ni kama hana Quality ya kuhudumu kwenye timu kubwa kama ile
Nikamuuliza kwa hiyo hadhi ya Mgunda ndio sababu ya kupata sare ya leo?
Nikamuambia ile mechi dakika za mwanzoni Simba ilicheza hovyo na mimi sikupendezewa kuona namna jinsi wachezaji hawajitumi kwa asilimia zote
Na kosa lililofanyika mpaka kupelekea Singida wapate bao la kuongoza, lilitokana na Enonga kufanya uzembe wa kucheza na mpira
Sasa hapo Mgunda anahusika vipi?
Haya kipindi cha pili Simba ilipiga mpira mwingi tukatengeneza nafasi nyingi lakini mwisho wa siku Kibu alikosa magoli zaidi ya matatu, hapo utamlaumu Mgunda kwa lipi?
Hili niliwahi kulizungumza hadi kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wanaona ule mfululizo wa kutoa sare kwenye mechi za kimataifa shida ni kochaHata ukirejea kutazama baadh ya mechi mfano vs Yanga, Azam, hao Singida na hata Mtibwa pamoja na kuwa walifungwa goli 5 lakini nafasi nyingi za kufunga magoli zilitengenezwa kwenye mechi zote hizo lakini washambulizi wanakosa umakini kabisa.. hii sio shida ya Mgunda amemuamini na kumpa nafasi kila mchezaji pale.. Wakati wake wa kulaumiwa apewe timu asajili silaha zake za maangamizi ashindwe ndio tuje kumlaumu hapa..
Na bahati mbaya viongozi wengi wa hizi timu wana mawazo ya kishabiki kama hayo na ndio mana mpira wetu unapata tabu sana kusonga mbele. Leo huko duniani Man City kapigwa na kumuacha Arsenal kubaki kileleni na watu wenye weledi na taaluma zao huwaoni wakitapatapa tazama hapa sasa Simba imeshinda leo kwenye mechi ngumu sana anatoka mtu anamlaumu kocha mara ooh timu inashika mkia tunashindaje goli moja sijui mara wametusumbua wanashindwa kuelewa hii ndio football.Hili niliwahi kulizungumza hadi kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wanaona ule mfululizo wa kutoa sare kwenye mechi za kimataifa shida ni kocha
Niliwakumbusha kuwa katika mechi yao na Zalan, Mayele alikosa magoli mengi ya wazi katika kipindi cha kwanza.
Lakini mechi ilivyomalizika kwa kufunga hattrick hakuna yeyote aliyeongelea zile nafasi alizokuwa anakosa kwasababu matokeo ya mwisho ni Yanga kashinda
Mechi waliotoa sare na Al Hilal bado Mayele alikuwa anakosa mabao ya wazi lakini, walipopata sare mashabiki walihamishia hasira zao kwa kocha
Wakati kilichokuwa kinaonekana uwanjani ni spirit ya wachezaji kwenye kujituma na kuipambania timu ilikuwa very low
Ukiwa na uongozi wenye watu wa mawazo kama haya ya mashabiki basi hatuwezi kufika mbali kwasbabu kila mechi tutayopoteza basi tutakuwa tunakazi ya kubadilisha makocha
japo simba imeshinda lakini bado inaitaji marekebisho mengi sanaFT: Simba SC 1-0 Ihefu FC
Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Ihefu FC.
90+3' kuelekea kumalizika kwa mchezo, Ihefu FC wanajitahidi kadri ya uwezo kutafuta bao, lakini muda mchache sana.
89' Akpan ameingia kuchukua nafasi ya MTUWilliam anaingia kuchukua nafasi ya Wadada
85' Sakho anafanya Kazi nzuri lakini, Simba wanashindwa kumalizika nafasi ile.
81' Kanoute anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya.
78' Kissu yupo chini akipatiwa matibabu, anatolewa nje, mpira unaendelea
72' Ihefu FC wanapata Kona ambayo haikuzaa bao, inaokolewa na Henock
67' Ssituba anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Kibu, ni faulo kuelekea Ihefu FC anapiga Kapombe, Kanoute anapiga kichwa njee.
63' [emoji460] SAKHO GOOOOOOOOOOOOOAAAL GOOAL, Pepe Sakho anaandika bao la kwanza kwa Simba SC
59' Ametoka Kyombo na ameingia Kibu.
57''Wadada anapiga Krosi lakini golikipa Manula anadaka bila wasiwasi
54' Sakho anafanya faulo, anaonywa na mwamuzi.
Tigere na Tshihimbi wanakwenda benchi na wameingia John na Kitenga.
Simba wameanza kwa kasi kipindi hiki cha pili kutafuta bao
49' Kyombo anakosa nafasi nzuri ya kufunga shuti lake linatoka sentimita chache ya lango la Ihefu
47' Kipindi cha pili kimeanza huku Simba wakifanya majaribio lakini Hussein anashindwa kuunganisha kichwa cha Phiri.
45+1' Kuelekea kuwa mapumziko.
Naaam mpira ni mapumziko na hakuna Timu imeona lango la mwenzake.
30’ Kipa wa Ihefu ameumia mchezo umesimama kwa muda, ameinuka mpira unaendelea
26' Simba SC wanapata faulo kwa mara nyingine, anapiga Okrah lakini anakosa nafasi nzuri ya kufunga.
Ni mpira wa kutengwa tena kuelekea Ihefu FC, Refa aliamuru mkwaju wa penalty, lakini alipata usaidizi wa mwamuzi wa pembeni.. Phiri anapiga shutii njee!
Simba wanapata Free Kick, anakwenda kupiga Okrah, anapiga shutii lakini linababatiza msitu wa mabeki.
15’ Simba wanaongeza mashambulizi lakini Ihefu wanakuwa wagumu kulinda lango lao
10’ Kasi ya mchezo inazidi kuongezeka huku kila timu ikijaribu kutafuta bao.
06' Simba wanaendelea kujipanga kwa pasi kadhaa huku wakitafuta mpenyezo nyuma ya mabeki.
04' Mchezo umesimama kwa muda, kiungo Tshishimbi wa Ihefu ameumia
03' Timu zinasomana, Simba wanapanga mashambulizi
00' Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa | Simba SC 0-0 Ihefu FC
View attachment 2414692
Kikosi cha Ihefu dhidi ya Simba, leo Jumamosi Novemba 12, 2022
View attachment 2414664
Kikosi cha Simba kinachoanza mchezo wa leo Novemba 12, 2022
dhidi ya Ihefu FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa
==============
Kama si Patashika basi ni Mbiringe ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kuvurumishwa leo Jumamosi ya November 12, 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC[emoji881] yupo tayari kuwakabili vilivyo Ihefu FC kwenye Uwanja wa Stade de Benjamin Mkapa[emoji2522] Jijini Dar es salaam.
Haya ndo maneno ya Makocha wa Timu zote mbili wanaelezea utayari wao namna watakavyozipambania alama tatu muhimu za Ligi Kuu Tanzania Bara
Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda amesema haya kuelekea mchezo huo muhimu.
Tunajua kesho (leo) tuna mchezo muhimu sana, maandalizi yapo vizuri na tupo tayari kupambana na Ihefu FC". Amesema Mgunda Gerdiola.
Kocha Msaidizi wa Ihefu FC Themi Felix amesema haya kuelekea mchezo huo muhimu.
Tupo tayari kwa mchezo dhidi ya Simba SC, ni kweli tupo mwisho na tuna mechi ngumu kesho (leo) lakini ukiangalia michezo yetu ya mwisho kuna mabadiliko". Amesema Themi Felix
Je..Nani mwenye mbinu Mujaarabu kwenye mawindo yake ya kuzipambania alama tatu muhimu? Ngoja Tusubiri Kuona Ndani ya Dakika 90 za Jasho na Damu.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa[emoji354] 1:00 Usiku.. Usikose Ukaadithiwa Yaani.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
PovuAmshukuru sakho kwani huyo sakho mchezaji wa mihogo fc,,, unavyosikia simba na huyo sakho ni sehemu ya simba, we uto vipi!
Unapenda muhogo?Amshukuru sakho kwani huyo sakho mchezaji wa mihogo fc,,, unavyosikia simba na huyo sakho ni sehemu ya simba, we uto vipi!
Unapenda muhogo?
Sasa hivi tuna majeruhi wengi karibu I kila mechi tuna majeruhi hatuna kocha wa mazoezi hii inaweza kuwa sababu inayochangiaViongozi wapo hadhiri (wanakusikia). Sehemu gani kwa mtazamo wako ambayo unaona pafanyiwe marekebisho..! Nguvu Moja [emoji881]
Wapi nilipoandika hivyo? Afu mbona ka una vielement vya mchele mcheleUnapenda muhogo?
Mnapoint zetu tatu mzunguko ujao msipo sajiri JanuaryUngeweka hela sasa
Na usikute uliibetia Simba ila huku mtandaoni ukija unavimba kudai kuipinga wakati mlo wako wa kesho umesababishwa na Simba
Unasema wabovu at the same time unaogopa kutia mzigo?
Umecheza mechi ngapi mpaka unaongoza ligi?
Na huyo unayemtambia, amecheza mechi ngapi?
Mambo Ashura Cheupe?Simba akishinda niiteni ASHURA CHEUPE
Kuna mambo Simba SC wanatakiwa kupambana kwa haraka na si kuchelewa kufanya hasa kuhusu haya ya Kocha wa mazoezi na Kocha wa makipa.Sasa hivi tuna majeruhi wengi karibu I kila mechi tuna majeruhi hatuna kocha wa mazoezi hii inaweza kuwa sababu inayochangia