FT: Simba SC 1-0 Vipers SC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa Stadium | 07.03.2023

FT: Simba SC 1-0 Vipers SC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa Stadium | 07.03.2023

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Leo majira ya saa 1:00 usiku, katika dimba la Benjamin Mkapa, Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa wanawakaribisha Vipers Sc katika mchezo muhimu sana.

Huu ni mchezo ambao Simba anahitaji alama zote 3 kwa hali na mali ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu kwa raundi ya robo fainali.

Je ile kauli ya kwa mkapa hatoki mtu itarejea tena leo? Naamini itarejea na Simba ataibuka na ushindi mnono.

Simba atashuka dimbani akiwa ana alama 3 huku vinara wa kundi hilo Raja wakiwa na alama 9 na wao watashuka dimbani ugenini muda mmoja kucheza na Horoya.

Kama ilivyo ada, mechi itakuwa mubashara, ZBC 2 ya AzamTv, Veriety 3 chaneli 228 ndani ya DStv na wale wa kustream basi utaipata mechi ndani ya YacineTv.com

Tukutane hapa saa 1:00 usiku

===
Vikosi vya mchezo wa leo

0CCE841A-EDDE-48EC-8B4D-3E74F8363813.jpeg

Kikosi cha Simba

829EF7B9-C6DF-4A6B-8483-9D06A3784C2E.jpeg

Kikosi cha Vipers SC
Mchezo unaanza
5' Kasi ya mchezo si kubwa
10' Simba wanatengeneza mashambulizi kadhaa
20' Vipers SC nao wanaonekana wapo imara, wamepata kona kadhaa
35' Simba wanapata nafasi kadhaa lakini hawazitumii vizuri
40' Saido anapiga shuti linapanguliwa na kipa
44' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Chama anafunga kwa shuti la mguu wa kushoto
45' Zinaongezwa dakika 4

MAPUMZIKO
FqoebHWXgAAVfTS.png

Kipindi cha pili kimeanza
48' Vipers wanaweka mpira wavuni lakini inakuwa offside
52' Wageni wanamiliki mpira na kushambulia lango la Simba
57' Bado Vipers wanaonekana kuwa na kasi kuliko Simba
70' Moses Phiri wa Simba anapata kadi ya njano
74' Phiri anatoka anaingia Baleke
90' Zinaongezwa dakika 4
90+4' Mwamuzi anamaliza mchezo
FULL TIME
 
benzema: I don't know what is going between Yanga and feisal..i think what has happened is disrespectful to Yanga hence Liverpool will pay for it next game
 
Back
Top Bottom