FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, tarehe 05.11.2023 iliyokuwa ikisubiriwa na Watanzania wengi imewadia. Siku ambayo wapenzi wa soka watashuhudia Derby ya Kariakoo, miongoni mwa Derby bora kati ya zile zinazoheshimika barano Afrika.

Mechi hii itaanza muda wa saa 11:00Jioni.

Kaa nami katika uzi huu upate kushuhudia matukio mbalimbali
View attachment 2804860
Kikosi cha Simba
View attachment 2804861
Kikosi cha Yanga
Timu zinaingia uwanjani, mchezo utaanza muda wowote kuanzia sasa
Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Mkapa
2' Timu zinasomana, pasi za hapa na pale

3' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kennedy Musonda anaifungia Yanga goli kwa kichwa huru, akiwa katikati ya walinzi wa Simba
7’ Dickson Job anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Saido
8’ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kibu Denis anafunga goli kwa kichwa akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Saido
13' Timu zote zinaonekana kuwa na presha ndani na nje ya uwanja
22’ Fabrice Ngoma anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Azizi Ki
30’ Yanga wanamiliki pira muda mwingi
40’ Simba wanaonesha uhai na kujipanga
43’ Shambulizi kali langoni kwa Yanga, mpira wa Kapombe aliopiga kapombe unaokolewa
45' Simba wanafanya shambulizi lingine kali lakini Yanga wanaokoa


Kipindi cha pili kimeanza
57’ Kipa wa Yanga anamchezea faulo Kibu Denis
59’ Kibu anashindwa kurejea uwanjani, nafasi yake inachuliwa na Luis
64’ GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Maxi Nzengeli anafunga goli la pili kwa Yanga, akipiga shuti kali
Baleke anatoka anaingia Moses Phiri
72’ Musonda ametoka ameingia Clement Mzize
73’ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Azizi Ki anafunga goli la tatu kwa Yanga, ikiwa ni goli lake la 7 katika Ligi Kuu 2023/24
77' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Max anafunga goli la nne kwa Yanga
Hatimaye simba yakipata ilichokisitahili muda mrefu.
Mo, fukuza huyo kocha feki arudi kwao akaendelee kuuza matikiti maji Rio-de jenairo
 
Walikua wanalilia 5G ya Yanga wamelambishwa leo. Oooh bahasha bahasha bahasha nao wamepokea bahasha😂😂😂😂😂
Ni aibuu iliojeeeeee 🤣🤣🤣🤣🤣!

Manula akajifukize upyaaaa🤣🤣🤣!

Imedundaaaaa😂
 
Back
Top Bottom