FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

Mtaani kuna watu wanajitakia vilema visivyo na ulazima

Unakuta shabiki wa Uto anakusumbua kelele nyingiii bughdha kibao unakosa hadi raha

Ukimcheki mdomoni tayari ana pengo (clean sheet haipo) na mtaani wanamuita pengo.

Mtu kama huyu anaweza kuipa serikali sababu ya kuingia upya bungeni kutunga ibara nyingine ya sheria kwa ajili ya kuwalinda watu wa Yanga.
Hawa jamaa watatubeza mpaka siku tunafunga huu mwaka....

kudadadekiiii leo tumepigika sana aiseee.......yaani sio poa kabisa
 
Just a very bad day in the office, kama kipigo kweli tumetandikwa, tena tumetandikwa haswaa, hakika kupata usingizi usiku wa leo ni ngumu, ikibidi tutafute vidonge vya usingizi angalau vitusaidie kupitisha haya masaa ilimradi pakuche, na hata kesho pakikucha sijui tutakimbilia wapi...

Kazini itakuwa moto...

Mtaani patakuwa moto...

Kwenye daladala itakuwa moto...

Kujifungia ndani nako patakuwa pamoto labda usiwashe radio, wala kusikiliza TV, inshort ikibidi na masikio tuzibe tusisikie kelele za nje, vinginevyo hali ni mbaya...

Na hili baridi la leo Dsm, kweli mtihani tumepewa, tukiuvuka huu tutaamka wanaume zaidi ya jana...

All in all, potelea mbali, Simba SC Nguvu Moja...

Wacha upepo wa kisuli suli upite ..
Kuimba kupokezana, ukicheka ujue kuna kulia pia.
Hongera kwa kuyapokea maumivu.
 
IMG-20231105-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom