Hayawi hayawi sasa yamekuwa, tarehe 05.11.2023 iliyokuwa ikisubiriwa na Watanzania wengi imewadia. Siku ambayo wapenzi wa soka watashuhudia Derby ya Kariakoo, miongoni mwa Derby bora kati ya zile zinazoheshimika barano Afrika.
Mechi hii itaanza muda wa saa 11:00Jioni.
Kaa nami katika uzi huu upate kushuhudia matukio mbalimbali
Timu zinaingia uwanjani, mchezo utaanza muda wowote kuanzia sasa
Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Mkapa
2' Timu zinasomana, pasi za hapa na pale
3' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kennedy Musonda anaifungia Yanga goli kwa kichwa huru, akiwa katikati ya walinzi wa Simba
7β Dickson Job anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Saido
8β GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kibu Denis anafunga goli kwa kichwa akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Saido
13' Timu zote zinaonekana kuwa na presha ndani na nje ya uwanja
22β Fabrice Ngoma anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Azizi Ki
30β Yanga wanamiliki pira muda mwingi
40β Simba wanaonesha uhai na kujipanga
43β Shambulizi kali langoni kwa Yanga, mpira wa Kapombe aliopiga kapombe unaokolewa
45' Simba wanafanya shambulizi lingine kali lakini Yanga wanaokoa
Kipindi cha pili kimeanza
57β Kipa wa Yanga anamchezea faulo Kibu Denis
59β Kibu anashindwa kurejea uwanjani, nafasi yake inachuliwa na Luis
64β GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Maxi Nzengeli anafunga goli la pili kwa Yanga, akipiga shuti kali
Baleke anatoka anaingia Moses Phiri
72β Musonda ametoka ameingia Clement Mzize
73β GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Azizi Ki anafunga goli la tatu kwa Yanga, ikiwa ni goli lake la 7 katika Ligi Kuu 2023/24
77' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Max anafunga goli la nne kwa Yanga
87' Penati, Yanga wanapata
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Pacome Zouzoua anafunga kwa kumchambua Manula
90' Zinaongezwa dakika 3
FULL TIME