Kinachonishangaza pamoja na Yanga kuonekana kama imeshinda mechi nyingi kwa goli nyingi nyingi msimu huu, ila kumbe mpaka sasa tofauti yake ya magoli ya kufunga na Simba ni magoli 9 tu.
Kilichoiua Simba msimu huu ni kuruhusu magoli mengi, hadi Coastal amefungwa magoli machache na wakati amecheza mechi mbili zaidi. Pia kukosa magoli mengi ya wazi. Poor finishing. Wachezaji wanaonekana wana misuli ila hawana nguvu kabisa za kupiga mashuti, wakifika golini wanataka magoli ya kudonoa donoa.
Toka enzi za Robertinho, sijawahi kuona Simba wakifanya mazoezi ya kupiga mashuti golini kwa hiyo hii haipo hata katika mentality ya wachezaji.