FT | Simba SC 3-1 Mbeya City FC | CRDB Bank Federation Cup | KMC Stadium | 13.04.2025

FT | Simba SC 3-1 Mbeya City FC | CRDB Bank Federation Cup | KMC Stadium | 13.04.2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Simba SC watashuka dimbani leo saa 10:00 jioni kuwavaa Mbeya City katika mchezo wa Robo Fainali ya CRDB Bank Federation Cup, ukitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo huo utakuwa kipimo muhimu kwa Mnyama Simba SC ambao wanalenga kutinga hatua ya nusu fainali na kuweka rekodi ya kutwaa taji hilo msimu huu, huku Mbeya City nao wakisaka kushtua vigogo na kuendeleza safari yao ya mashindano.

1744531746783.png

Timu zimeingia na Vikosi hivi

1744550972715.png

1744551195262.png
Mechi imeanza

1' Faulo - Mbeya City wanapiga
2' Kona - Simba wanapiga
4' Kona - Simba wanapiga
5' Kona - Simba wanapiga
6' Kona - Simba wanapiga
8' Kona - Simba wanapiga
14' Faulo - Simba wanapiga
15' Ateba anapaisha juu ya lango
18' Ateba anapoteza nafasi
22' Gooal -Mbeya City (Mudathir Said)
24' Gooal - Simba SC (Ngoma)
29' Gooal - Simba SC (Ateba)
35' Kona - Mbeya City wanapiga
43' Goooal - Simba SC (Mutale)
45'+2 Kona - Simba SC wanapiga
45+5' Kadi ya Njano- Mbeya City (Said)

Dakika 5 zimeongezwa

HT:
Simba SC 3-1 Mbeya City FC
⚽️ F. Ngoma 24' | ⚽️ M. Said 22'
⚽️ L. Ateba 29'
⚽️ J. Mutale 43'

Kipindi cha pili kimeanza

45' Mabadiliko - Simba SC (Balua In - Chamou Out)
47' Mabadiliko - Mbeya City
48' Mechi imesimama Ateba anatibiwa
53' Awesu amepoteza nafasi
57' Kona - Simba SC wanapiga
61' Mabadiliko - Simba SC (Okejepha In - Hamza Out)
76' Mabadiliko - Simba SC (Mukwala In - Ateba Out | Kapombe In - Ngoma Out)
78' Mabadiliko - Mbeya City
87' Mabadiliko - Simba SC (Adolf Said [U20] In - Awesu Out)

Dakika 5 zimeongezwa

90+2' Kona - Simba SC wanapiga
90+2' Kona - Simba SC wanapiga

FT: Simba SC 3-1 Mbeya City FC
⚽️ F. Ngoma 24' | ⚽️ M. Said 22'
⚽️ L. Ateba 29'
⚽️ J. Mutale 43'

🏆 MOTM - Fabrice Ngoma
 
Simba Nguvu Moja
Mnyama mkali tukutane saa kumi jioni
 
Attachments

  • IMG_20250413_115404.jpg
    IMG_20250413_115404.jpg
    139.2 KB · Views: 43
Kocha wetu wa Simba tunaomba uwapumzishe baadhi ya wachezaji kwenye hii mechi. Kwa kweli unawatumia kupitiliza. Timu haina kabisa rotation!

Kuna baadhi ya wachezaji wetu mfano Mzamiru Yassin, Aishi Manula, Valentine Nouma, Okejepha, Debora Mavambo, Aweso Aweso, nk. wanaelekea kusahaulika kwa kukosa kabisa nafasi ya kucheza! Kwa nini huwaigi watani zetu Yanga ambao karibia wachezaji wao wote walio wasajili msimu huu wanapata nafasi ya kucheza hata kwa dakika chache!

All in all, naitakia ushindi timu yangu ya ukweni Mbeya City. 😩
 
Kocha anaogopa kupoteza, analinda kibarua.
 
Kama ningekuwa kocha.
1. Ally salum
2. Duchu
3. Agustine Nouma.
4 . Hamza
5. Karabue chamoe
6. Ngoma
7. chasambi.
8. Debora.
9. Ateba.
10. Awesu.
11. Mutale.
 
Sisi kama simba tunataka ushindi siyo rotation
 
Kocha wetu wa Simba tunaomba uwapumzishe baadhi ya wachezaji kwenye hii mechi. Kwa kweli unawatumia kupitiliza. Timu haina kabisa rotation!

Kuna baadhi ya wachezaji wetu mfano Mzamiru Yassin, Aishi Manula, Valentine Nouma, Okejepha, Debora Mavambo, Aweso Aweso, nk. wanaelekea kusahaulika kwa kukosa kabisa nafasi ya kucheza! Kwa nini huwaigi watani zetu Yanga ambao karibia wachezaji wao wote walio wasajili msimu huu wanapata nafasi ya kucheza hata kwa dakika chache!

All in all, naitakia ushindi timu yangu ya ukweni Mbeya City. 😩
Mzamiru ni majeruhi.

Makipa wanafanyiwa rotation vizuri tu, kuanzia Camara, Salim na hadi Abeli. Hata Yanga haina rotation ya makipa watatu, wewe unataka Simba iwe na rotation ya makipa wote wanne.

Nouma, Okejepha na Mavambo wanacheza ingawa ningependa kuwaona wakicheza zaidi. Nouma anamtoa sub hadi captain katika mechi muhimu. Eti unasema anasahaulika? Awesu naye anacheza sana tu.

Umewataja wote hao kwa kulazimisha ila lengo lako hasa lilikuwa ni Manula. Ana deni gani na nyie mbona mmegeuka watetezi wake? Kuna kazi gani mliyomtuma hajaimaliza?
 
Back
Top Bottom