Naaaam..!
Hujambo na Karibu kwenye Matangazo ya Habari za Michezo, Burudani na Uchambuzi.
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Jumamosi ya July 3, 2021, ambapo mchezo unaobeba hisia za mashabiki wengi Tanzania na nje ya Tanzania kati ya Watani wa Jadi, Kariakoo Derby, Simba SC dhidi ya Yanga SC. kukabiliana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba SC na Yanga SC ni Derby bora Afrika pamoja na zile za Orlando Pirates Vs Kaizer Chiefs, Ahly Vs Zamalek, Raja Vs Wydad, Club African Vs Esperance Tunis.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote ambapo Simba SC wakiwa katika nyakati bora kabisa huku Yanga SC wakipata matokeo mazuri mfululizo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na Timu ambayo wanakutana nayo lakini lazima washinde kwa sababu wanahitaji ubingwa.
"Nia yetu ni kutetea vikombe vyetu vyote, tunajua siku zote mechi ya Derby si rahisi na sisi kwa kutambua ugumu wake tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi". Amesema Matola.
Kocha wa magolikipa Razack Siwa, amesema kuwa wamejianda vizuri kupata ushindi mchezo wa leo
Tumejiandaa vizuri sana juu ya mchezo wa huu na hakuna asiyejua ukubwa wa Derby hii kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi, kwahivyo tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi". Amesema Siwa.
Endapo Simba SC watashinda mchezo huu, watakuwa Mabingwa wa Nchi kwa msimu huu wa 2020/21 kwa mara ya Nne mfululizo.Yote kwa yote dakika 90 za jasho na damu kuamua kwenye Uwanja wa Mkapa.
Kumbuka mchezo huu ni kuanzia saa 11:00 Jioni. Usikose Ukasimuliwa
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.
..... Ghazwat na Crew Mzima ya JF Karibu....