FT: Singida FG 1 - 1 Simba (PNT: 2 - 3) | Mapinduzi Cup Semi Final | Amani Complex | 10.01.2024

FT: Singida FG 1 - 1 Simba (PNT: 2 - 3) | Mapinduzi Cup Semi Final | Amani Complex | 10.01.2024

Ile ni kona sio kona ? Kama ni kona elezea

Kama sio kona elezea
Ile haikuwa kona kwa sababu hizi.

1. Mpira aliopigwa na Saido ulitoka nje, na kipa aliudakia nje.

2. Mshika kibendera alishaonyesha ni goal kick, sio kona. Ajabu ni mwamuzi kuamua kuwa ni kona.
 
Baadhi ya mashabiki wa kibongo ni kama mambuzi tu.

Kwenye ile mechi kati ya Simba Sc na Wydad kule ugenini ziliongezwa dakika ngapi? Na Simba Sc akaja kufungwa dakika ya ngapi?

Tulivyolalamika mashabiki wa Yanga Sc waliponda sana, ila leo kwakua haiko upande wao ndio wanaona tatizo?

Mimi sioni tatizo lolote kwa refa.
Ni kwa sababu afrika ni bara la hovyo
 
Mchezo umekwisha lakini makosa ya mwamuzi yamewacost Singida FG, Goli la Simba limepatikana dakika ya 98 wakati ziliongezwa dakika 6, 90+6=96.
Mapinduzi Cup wasipofikiria kutumia marefa wa nje, basi mashindano hayo yatakufa. Mwaka huu timu zote mbili zilizoingia fainali zimebebwa na marefa tu; kwa uhakika fainali halisi ilitakiwa kuwa baina ya APR na Singida
 
Dakika za nyongeza za kamisaa zilikuwa ni sita tu, na ndio kibao kilionyesha uwanjani. Azam walianza kwa kuweka kusema ni dakika 8 (sijui walielezwa na nani?) lakini kibao kilipoonyesha ni dakika sita na wao wakabadilisha na kuandika ni dakika 6.

Kuna Mchezaji wa Singida alijiangusha
 
Walalamikaji wengi wapo kihisia hata nilipowaomba ufafanuzi wa kilichotokea hakuna aliyejitokeza kutoa sababu ya maana

Hii inafanya ionekane watu ambao hawajaona mpira washindwe kujua nini kimefanyika

Na pointi hiyo inapoteza maana halisi ya live updates kama vitu sensitive kama hivi vinaishia gizani na watu tunaowategemea kutoa ufafanuzi wapo kihisia
Ukweli ni kwamba umeona Mechi Kwa hiyo kilichotokea unakijua. Mimi ningekuwà na uhakika hujaona Mechi ningekuhadithia.
 
Back
Top Bottom