FT| Tabora United FC 0-3 Simba SC | NBC Premier League | Ali Hassan Mwinyi Stadium | 02-02-2025

Joshua Mutale atumie hizi mechi zisizo na presha kutulia na kutafuta kiwango kama kipo badala ya kukimbia kimbia.

Narudia tena..sioni

Hujui mpira..hii mechi haikuwa na presha?!

Usikurupuke mkuu, angalia muda mutale alioingia na Simba ilikuwa ikiongoza goli ngapi halafu jihitimishie kuwa presha kama ilikuwepo au la.
Kuna kitu kimoja kimeanza kunipa matumaini kwa Mutale. Sasa hivi hana mambo mengi uwanjani, anagusa anaachia. Hii ndiyo njia ilitumika kumrudisha Kibu kipindi kile alipokuwa anazingua.

Mchezaji anapokuwa amevurugwa, inabidi arudi kwanza kufanya mambo basic tu, halafu confidence ikirudi taratibu na wenge likishatoka ndiyo unamwambia aanze kurudisha vitu vingine taratibu katika uchezaji wake.

Jamaa nilishamkataa ila naanza kupata matumaini.
 
Bado hatujapata mbadala wa Chama. Ahoua ana makosa makosa mengi mno.
Sahihi. Ahoua zaidi ya penati baaaado saaana. Nadhani hata faulo awe anapiga Kibu maana Ahoua hata kuvusha mpira kwenye ukuta bila kupaisha hawezi.
 
Reactions: Tsh
Your browser is not able to display this video.

Kamdomo kanaponza , jamaa aomba msaada Kwa shetani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kweli mkuu.
 
Sahihi. Ahoua zaidi ya penati baaaado saaana. Nadhani hata faulo awe anapiga Kibu maana Ahoua hata kuvusha mpira kwenye ukuta bila kupaisha hawezi.
Kuna muda anakuwa vizuri, kuna muda anakuwa wa kawaida kama vile si mchezaji tegemeo wa club kubwa kama Simba. Anyway, muhimu timu inashinda.
 
Kuna muda anakuwa vizuri, kuna muda anakuwa wa kawaida kama vile si mchezaji tegemeo wa club kubwa kama Simba. Anyway, muhimu timu inashinda.
Jana aliharibu move zisizopungua mbili za magoli. Labda tumvumilie maana unaweza kusema bado anatengeneza game yake
 
Reactions: Tsh
Jamani mimi ndo naangalia marudio ya hii mechi...
-Niliyoyashuhudia kwny hii mechi...
-Simba ni ya motooooo...
-Tabora wana timu ila wameshindwa mziki mnene wa simba pamoja na mbinu Za FD Ila hawa nyuki watawachachafya watu timu wanayo...
-Yani sub ya Simba nje moto ndani moto..yani hii ndo inaitwa ndani ntiti nje ntiti
-Aisee Mutale anakuja vzr haswaa anatoa pasi kwa wakati..
-Mpanzu ni mtu na nusu
-Huyu Nouma ni balaaa sema shabalala kinambeba ni uzoefu
-Debora kaanza kutoa pasi zenye macho yuko vzr haswaaa...
-Mukwala anakosa finishing tuu yaniii ila ana bahati na lango...
-Camara dhambi zake apewe boka....
-Chasambi mtoto ana balaa huyu...
-Ateba atawaua ..

SIMBA BINGWAAAAAAAAAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…