FT: Vipers S.C 0-1 Simba S.C | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 25.02.2023

FT: Vipers S.C 0-1 Simba S.C | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 25.02.2023

utopolo og

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
575
Reaction score
1,575
Ni siku nyingine tena ambapo Mabingwa wa Uganga Vipers S.C wanawakaribisha Simba S.C kwenye mchezo mwingine wa kutafuta alama tatu ili kujiweka sawa katika msimamo wa kundi C wa ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la mtakatifu Maria huko Kitende nchini Uganda.

Ikumbukwe kuwa Simba ndio vibonde wa kundi hili wakiwa mkiani mwa kundi bila point yoyote huku wakiwa hawajafunga goli lolote, hivyo wataingia wakiwa na kiu ya kupata ushindi ili angalau waweze kufufua matumaini ya kufuzu hatua inayofuata.

Kwa upande wa wenyeji Vipers wao pia Hali yao sio nzuri japo wana point moja hivyo ushindi kwao ni muhimu ili kuendelea kuwa na ndoto za kutinga robo fainali.

Je, mnyama atapindua meza ugenini? Au vipigo vitaendelea? Majibu yatapatikana ndani ya dakika 90.

Mchezo huu utapigwa majira ya saa 1.00 usiku wa leo na utakuwa mubashara kupitia ZBC2 ya Azam Tv na channel 229 ya Dstv

Muda wowote refarii atapuliza Kipyenga kuashiria kuanza kwa mechi.........

Screenshot_20230218-211423.jpg
imgonline-com-ua-resize-UrZfQU3627-scaled.jpg
matokeo-simba-raja-full-810x544.jpg
Screenshot_20230225-183924_Twitter.jpg


======


00" Mpira umeanza hapa Uwanja wa St Mary's Vipers ndio wanakuwa wa kwanza kugusa boli

06" Shambulizi kali hapa linafanya na Simba langoni mwa vipers lakini shuti la Clautos Chama linatoka sentimita chache na kwenda nje

08" Moses phiri anapiga shuti kali linaokolewa na golikipa wa vipers na kuwa kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.
Simba wameanza kwa kasi sana mchezo huu na inaonekana wanazitaka point tatu kwa udi na uvumba.

10" Milango bado migumu kwa timu zote mbili

14" Hatari langoni mwa Simba ila mpira unaenda nje. Vipers wamefanya Shambulizi zuri lango la Simba

19" Gooooooooooal. Simba wanapata bao la kuongoza lililofungwa na Enock Inonga baada ya mpira wa faulo uliopigwa na Mohamed Hussein.
Vipers 0-1 Simba S.C

30" Bado Simba iko mbele kwa bao 1

35" Vipers wanafanya Shambulizi kali langoni mwa Simba ila shuti la Karisa linapanguliwa na Aishi Manula. Yupo chini Manula baada ya kufanyiwa faulo

45" Kapteni wa Vipers Milton Karisa anatoka nje baada ya kupata majeraha na nafasi yake inachukuliwa na Orit.

45+3" Zimeongezwa Dak tatu kuelekea mapumziko
Ni Half timu Mnyama mkali Simba anakwenda mapumziko akiwa mbele Kwa goli Moja

Dakika 45 za kipindi cha pili zimenza hapa katika uwanja wa Mtakatifu Maria-Kitende

50" Vipers wamekuja moto sana hiki cha pili wanatafuta bao la kusawazisha

54" Enock Inonga beki wa Simba anaoneshwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya

60" Mabadiliko upande wa Simba, anatoka Moses phiri anaingia Erasto Nyoni.

70" Simba bado ipo mbele kwa lilelile goli moja

81" Mabadiliko Kwa upande wa Simba, Kibu Denis anatoka, anaingia Habib kyombo

90" Simba wanapoteza muda ili kukamilisha muda maana wako mbele Kwa bao Moja

90+5 Zimeongezwa tano za kufika muda uliopotea.
Kwa namna inavyoonekana Simba wanaondoka na ushindi hapa katika uwanja wa Mtakatifu Maria.

Muda wowote refarii atapuliza filimbi kuashiria kutamatika kwa mpambano huu

Naam mpira umekwisha. Mnyama mkali Simba anaondoa na ushindi wa goli Moja lililofungwa na Enock Inonga.
Hadi wakati mwingine alamsiki.
 
Pilipili FC leo wataishia kulialia tena, kama ilivyo kawaida yao. 😁
 
Ni siku nyingine tena ambapo Mabingwa wa Uganga Vipers S.C wanawakaribisha Simba S.C kwenye mchezo mwingine wa kutafuta alama tatu ili kujiweka sawa katika msimamo wa kundi C wa ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la mtakatifu Maria huko Kitende nchini Uganda.

Ikumbukwe kuwa Simba ndio vibonde wa kundi hili wakiwa mkiani mwa kundi bila point yoyote huku wakiwa hawajafunga goli lolote, hivyo wataingia wakiwa na kiu ya kupata ushindi ili angalau waweze kufufua matumaini ya kufuzu hatua inayofuata

Kwa upande wa wenyeji Vipers wao pia Hali yao sio nzuri japo wana point moja hivyo ushindi kwao ni muhimu ili kuendelea kuwa na ndoto za kutinga robo fainali.

Je mnyama atapindua meza ugenini?
Au vipigo vitaendelea?
Majibu yatapatikana ndani ya dakika 90

Mchezo huu utapigwa majira ya saa1.00 usiku wa leo na utakuwa mubashara kupitia ZBC2 ya Azam Tv na channel 229 ya Dstv

N.b Hela za mama Samia bado zipoView attachment 2529472View attachment 2529473View attachment 2529474
Nasimama na SIMBA yangu
6f58edfbac18c337bb6e80276d57fc7b.jpg
 
Back
Top Bottom