FT: Vipers S.C 0-1 Simba S.C | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 25.02.2023

FT: Vipers S.C 0-1 Simba S.C | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 25.02.2023

Ni siku nyingine tena ambapo Mabingwa wa Uganga Vipers S.C wanawakaribisha Simba S.C kwenye mchezo mwingine wa kutafuta alama tatu ili kujiweka sawa katika msimamo wa kundi C wa ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la mtakatifu Maria huko Kitende nchini Uganda.

Ikumbukwe kuwa Simba ndio vibonde wa kundi hili wakiwa mkiani mwa kundi bila point yoyote huku wakiwa hawajafunga goli lolote, hivyo wataingia wakiwa na kiu ya kupata ushindi ili angalau waweze kufufua matumaini ya kufuzu hatua inayofuata

Kwa upande wa wenyeji Vipers wao pia Hali yao sio nzuri japo wana point moja hivyo ushindi kwao ni muhimu ili kuendelea kuwa na ndoto za kutinga robo fainali.

Je mnyama atapindua meza ugenini?
Au vipigo vitaendelea?
Majibu yatapatikana ndani ya dakika 90

Mchezo huu utapigwa majira ya saa1.00 usiku wa leo na utakuwa mubashara kupitia ZBC2 ya Azam Tv na channel 229 ya Dstv

N.b Hela za mama Samia bado zipoView attachment 2529472View attachment 2529473View attachment 2529474
Kwenye picha kikosi Cha vipers kinaonekana kipo imara zaidi...

Sisi NDIO Simba 🦁🦁 Nguvu moja tuna fyeka Kila kisiki kitakacho kuja mbele....

Mungu ibarik Simba 🦁🦁 MUNGU ibarik Tanzania

Leo vipers lazima wapoteane....
 
Hivi nyie Utopolo kushinda ile game ya michuano ya LUZA mnajiona kama nina, mbona hamtaki Simba iwe na Amani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] [emoji23] Sasa muwe na amani ya kazi gani?
Waganda ni ndugu zetu kabisa, Kila la kheri waganda
 
Bado masaa machache tuanzw kusikia hizi kauli

"Hamna kocha humo"

"Mo tapeli tu"

"Bocco Mzee anarogq wenzake"

" Mgunda alikua kashaipatia timu mzungu anaharibu"

"Hongera kwa wale wanaoihujumu timu"

" Mangungu anatakiwa aachie uongozi"

" Manula nae kiwango kimeshuka"

" Hawa jamaa kwa mkapa wakija hawatoki"

" Chama hatakiwi kucheza winga anatakiwa acheze kati pale"

" Sawadogo tumepigwa"

" Kwanini tumemuacha mkude dar"

" Sakho anarukarukq tu"

" Kocha ampe nafasi Kibu Dee"
 
Hayo matokeo yawekwe juu chini.
Uwanja wa St. Mary's huwa wanatoka, ila wanaenda kulala na viatu..
Kwetu tuna wakwe zetu Waganda, lazima niwaunge mkono wakwe.

#Lolote linaweza kutokea...
kesho sio mbali, ni bora tuwaombee tu, hata droo sio mbaya
 
Ni siku nyingine tena ambapo Mabingwa wa Uganga Vipers S.C wanawakaribisha Simba S.C kwenye mchezo mwingine wa kutafuta alama tatu ili kujiweka sawa katika msimamo wa kundi C wa ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la mtakatifu Maria huko Kitende nchini Uganda.

Ikumbukwe kuwa Simba ndio vibonde wa kundi hili wakiwa mkiani mwa kundi bila point yoyote huku wakiwa hawajafunga goli lolote, hivyo wataingia wakiwa na kiu ya kupata ushindi ili angalau waweze kufufua matumaini ya kufuzu hatua inayofuata

Kwa upande wa wenyeji Vipers wao pia Hali yao sio nzuri japo wana point moja hivyo ushindi kwao ni muhimu ili kuendelea kuwa na ndoto za kutinga robo fainali.

Je mnyama atapindua meza ugenini?
Au vipigo vitaendelea?
Majibu yatapatikana ndani ya dakika 90

Mchezo huu utapigwa majira ya saa1.00 usiku wa leo na utakuwa mubashara kupitia ZBC2 ya Azam Tv na channel 229 ya Dstv

N.b Hela za mama Samia bado zipoView attachment 2529472View attachment 2529473View attachment 2529474
Kwenye hiyo picha ya vipers Kuna huyo jamaa wa kushoto kwao kavaa kitambaa Cha uongozi huwa ana tuvurugu vurugu Fulani kwenye pitch,yawapasa Madunduka kuwa na tahadhari zote. Kila la Kheri Milton Karisa!
 
SeMBe gufu moiyah.
Kwa Mtakatifu Mariamu hatoki mtu.
Leo rasmi tunaanza safari yetu ya kubeba kombe la robo fainali.
 
Back
Top Bottom