FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

Halafu mbona Inonga kama anambania sana Outtara? Mfano game ilopita
 
Kwenye biashara hasara huwa zipo lakini Yanga kwa Aziz Ki ni hasara kubwa kuwai kotokea.
 
Watani wakishinda hii mechi tusilaumu wamebahatisha ,wana Morison ,Aziz K ,Bangala ,Aucho, Djuma ,Feisal ,Mayele ,unaona wamekamilika halafu unawapanga Kanuti na Israel Mwenda,... Rubbish ,Kipindi cha kwanza striker ni Kibu tu
Hao jamaa unaowazarau hadi sasa kipindi cha kwanza wamecheza vizuri.ngoja tusubiri kipindi cha pili.
 
Goooh;Simba,Simba,Simba hakuna cha Mayele.
Timu zote zimeshaingia uwanjani.

Mchezo umeanza

01' Yanga wanamiliki mpira wakipiga pasi kadhaa.

11' Kibu Denis anaachia mkwaju na kuishia kwenye nyevu za pembeni

15' ⚽Gooooooal, Pape Sakho anaweka kimiani goli la kwanza la mchezo, krosi maridadi kutoka kwa Chama

19' 🟨Aucho anapewa kadi ya njano

22' Kona ya kwanza ya mchezo inachongwa na Yanga, almanusura Aziz Ki aweke uwanja sawa

23' Inonga anamjaribu Diarra kutoka nje ya 18 lakini anakuwa makini na kuupangua nje

24' Mohammed Hussein anachonga kona ya kwanza ya Simba, mpira unakosa manufaa

33' Feisal anaenda chini baada ya kukwatuana na Mkude, free kick ya Yanga inashindwa kuleta matokeo kwa kuleta offside

37' Simba wanapata freekick nje kidogo ya 18, Kanoute anajaribu kuunganisha krosi ya Chama lakini Diarra yuko makini.

42' Mlinda mlango wa Simba yuko chini akitibiwa maumivu ya misuli

45+1' Inonga anainua kiatu juu ya Sureboy, inapulizwa filimbi na zogo linatokea

45+4' 🟨Sureboy anapewa kadi ya njano kwa kumletea ubabe Inonga

45+4' 🟨Inonga anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Abubakar Sureboy


=========


Tarehe imewadia.
Klabu mbili kubwa hapa nchini zinaenda kukiwasha uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana walipokutana kwenye ngao ya jamii Yanga alipata ushindi wa goli moja lililofungwa na Fiston Mayele.

Je, mnyama mkali atalipiza kisasi au Yanga ataendeleza ubabe? Tutakuwa hapa kupeana taarifa.

Mchezo utaanza saa moja kamili jioni.

=============
Timu zote zimeshawasili Uwanja wa Mkapa.

Kikosi cha Simba
Kikosi cha Yanga cha leo

Timu zilipokuwa zikiingia uwanjani mapema leo:
 
Back
Top Bottom