FT: Yanga 3-0 Tabora United | CRDB Bank Federation Cup | Azam Complex | 01.05.2024

Nimegundua Utopolo ni Mbumbumbu+ na ndo maana walizolewa na upepo. Ukweli ni kwamba ile hukumu haimhusu Mchezaji bali klabu. Kwenye uhamisho wa Mchezaji, timu inayonunua Mchezaji inaweza kukubaliana na timu inayouza Mchezaji kulipa Ada ya Uhamisho kwa awamu. Sasa hayo makubaliano huwa yanasimamiwa na FIFA ili kuhakikisha Mdaiwa analipa. Ukichelewa kulipa ndo unakumbana na lile rungu walilopigwa Uto kama njia ya kuwashikiza. Makubaliano haya hayamhusu kabisa Mchezaji kwa sababu mchezaji anakuwa na makubaliano yake na timu mpya na klabu ya zamani na yenyewe huwa na makubaliano yake na klabu mpya. Na klabu zikishakubaliana tu kuhusu kulipana kwa awamu, Mchezaji husika anakuwa Mchezaji Halali wa klabu mpya na ataidhinishwa, na yatakayotokea baadae yeye hayamhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…