FT: Yanga SC 1-1 Simba SC | Ligi Kuu NBC '22/'23 | Benjamin Mkapa Stadium

FT: Yanga SC 1-1 Simba SC | Ligi Kuu NBC '22/'23 | Benjamin Mkapa Stadium

Mpira utaisha kwa droo ya 1:1 lakini mmoja wao atasawazisha dakika za majeruhi
 
Naaam, wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika. Pambano lenye hadhi la watani wa jadi katika soka la bongo, Yanga na Simba.

Karibuni katika matukio mubashara (live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa soka la Bongo #KariakooDerby Yanga na Simba, utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa leo jumapili 23-10-2022.

Huu ni mchezo wa namba 64 wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023, Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.

Mchezo uliyopita wa Ligi Kuu msimu wa 2021/2022 uliochezwa April 30, 2022, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/suluhu ya 0-0. Kwa maana hiyo huu ni mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye msimu wa 2022/2023.

Timu hizo zinaingia uwanjani zikiwa na alama 13 kila moja, lakini Simba ipo kileleni kutokana na wingi wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili, kila moja amecheza mechi tano.

Pia michezo mingine (Derby) ya hivi karibuni ni ule wa Mei 28, 2022 kwenye nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup ambapo, Simba alifungwa goli moja bila majibu, ambapo shuti kali la Feisal Salum ‘Fei Toto’ liliwalaza na viatu mashabiki wa Simba siku hiyo.

Vilevile mnamo Agosti 13, 2022 kwenye mechi ya ngao ya Hisani, Simba alitepeta tena kwa Yanga kwa kufungwa goli 2 kwa moja. Fiston Mayele "Mzee wa kutetema" akiingia kambani mara mbili siku hiyo na mashabiki wa Simba wakitoka vichwa chini.

Kwa miaka ya karibuni Simba imekuwa ikishindwa kupata ushindi mbele ya Yanga katika michezo ya Ligi Kuu Bara kwani mara yao ya mwisho kushinda ilikuwa bao 1-0, Februari 16, 2019 lililofungwa na mshambuliaji, Meddie Kagere.

Kwenye mechi za kimataifa, tarehe 16/10/2022 Yanga imetolewa kwenye michuano ya CAF CL na Al Hilal baada ya kufungwa 1-0 na kushukia kwenye michuano ya CAF CC ambapo pia amepangiwa Club Africain kwenye mchezo wa Play off kuelekea makundi.

Pia Simba mechi ya mwisho kimataifa imetoka kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufuzu hatua ya makundi ya CAF CL.

Je, leo itakuwaje baina ya miamba hii miwili? Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Azam Sports 1 HD wataurusha mpambano huu mubashara (live).

Je, "Watatetema" au "watapiga saluti?" Hahaha #𝑯𝒂𝒊𝒏𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂
Pamoja ya kuwa umetumia font mbovu, kila la heri kwa Mnyama leo🦁🦁🦁
 
Simba hii gemu anafungwa tukiwakosa na hawa basi hakuna Timu tutaifunga mwaka huu...ngoja wafunguke kama walivyocheza na wale wabovu tuwaue..
 
Mhhhh kisa cha kutolala?.yani saa sita uzi tayari yani leo kipigo kwa gongowazi hakiepukiki
 
Back
Top Bottom