Hivi Koran imeshindwa kiasi cha kutaka isaidiwe na mahakama?
Heheee, kazi kweli haya maswali mengine, lakini sawa tutajaribu kukuelewesha.
It seems to me from your question, or let us say, Are you really serious that you don't understand what or the difference between Koran, Mahakama (courts) and "Sharia" are, even in their simple lay terms? Unbeleivable but may be possible. If truly you don't understand these terms then may the Almighty bestow you with the knowledge, most importantly the understaning.
"Koran" ndugu yangu ni maneno ya Mwenyezi Mungu (SW) aliyomteremshia Mtume wake Muhammad (SW) ambayo kwa uwezo wake yeye mwenyewe Mwenyezi Mungu amewezesha maneno yake hayo kuhifadhiwa katika kitabu kiitwacho msahafu/Koran au kuhifadhiwa kama yalivyoteremshwa ndani ya nyoyo/akili za baadhi ya waja wake wenye kuamini (waislamu). Kwa mfano ni kama vile Zaburi (Psalms) kwa Daudi(David), Tauarati (Torah) kwa Musa(Moses) , Injili (Gospel) SIYO Biblia/Bible, tafadhali tofautisha vizuri, kwa Yesu(Jesus). Mpaka hapa nafikiri unapata picha kwamba vitabu vitakatifu hivi kwahivyo huwa kwa wakati na watu husika ndio "Source of reference" ya masuala yao yote na yote ya maisha. Nyengine ni Sunna (somo jengine hili lakini kwa kifupi hii ni "source of reference" katika uislamu ambayo inatokana na Mtume Muhammad (SAW)). Katu "Source" hizi hazishindwi hata siku moja na zina majibu na maelekezo ya maswala yote, yote na yote ya maisha ya mwanadamu, labda ni watu ambao kwa ujinga, kutokupenda au kupenda dunia zaidi ndio hushindwa kuvifuata.
"Sharia" mdogo wangu ni hukumu mbali mbali kwa mujibu wa "source" yaani hapa Koran, zinazoongoza uundaji na utekelezaji wa jambo lolote linalomuhusu mtekelezaji. Wewe ndio tuseme huna muislamu unaemfahamu ambae anatekeleza masuala yake ya dini kama kuswali, kufunga, kudai kitu fulani halali na akakitumia na kenginecho haramu na akajiepusha, nk, nk. Huna mtu wa namna huyo? Naam, basi anafuata "Sharia" katika individual level. "Sharia" haiishii katika individual level tu bali hutanuka mpaka katika family level, village, nation mpaka international level. Kama "source" ya utekelezaji wa jambo fulani ni Koran, iwe mfano kifamilia/kijamii: ndoa/mirathi, iwe ki-national level (mfano MAHAKAMA/Taifa/Dola(Nation/state), vita dhidi ya madhalimu na wavamizi, iwe kimataifa, eg. haki za binadamu, za wanawake na watoto nk, nk, basi jambo lile husemekana limefanywa kwa mujibu wa "Sharia". umeelewa???
Hivyo hapo Koran itashindwaje? Au inakuwakuwaje hata Mahakama iwe replacement ya Koran iliyoshindwa? Inawezekana kweli?
Kwa kifupi tu Mahakama, Majlisi Shura (mfano wa bunge/wakilishi), na vengine vingi ni vyombo tu vya uundaji na utekelezaji wa "Sharia" kwa mujibu wa sources "Koran" na "Sunna" ambavyo ni maelekezo ya Mwenyezi Mungu (SW) aliyoyawezesha kuhifadhika daima na milele ili vipate kubainisha uhalali, uharamu, kiasi, nk kuhusiana na kila aspect ya maisha ya mwanadamu at individual, family, village, nation and global level.
Remember, Mahakama ya kadhi wanayoitaka waislamu ni ile itakayoshughulikia masuala ya "civil" tu na siyo "Criminal" unless labda serikali ishindwe ku-deal na mafisadi na wawatake waislamu watanue zaidi na kuwashughulikia ki"criminal" mafisadi. Ufisadi lazima uwe mwisho. Wanalijua hilo!!!