Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account


Sheria ipi ya Tanzania ambayo haimpi mtuhumiwa haki ya kutoa utetezi wake?
 
Nani anaamini Pinda kama waziri mkuu kesho atatangaza kujiuzulu
 
Naongelea uwasilishaji, si huo uchunguzi. Na pia tumesikia upande mmoja mpaka tungoje upande wa pili wanasemaje.

Mpaka sasa sijaona kilichowasilishwa ambacho hakijibiki.


Leo Bi mkubwa naishia hapa. Game over. Ni haki yako kuamini unachokiona sawa kwako, hawa wataishia kusema

-Tumedhalilishwa sana

-Tumenyanyaswa sana

-Tumeonewa sana

-Tumesoneshwa sana nk, nk nk

Halafu mwisho wataishia kutimuliwa au kujiachia mitini na kushuka pwaa aridhin na kupasuka mithili ya dafu lilooza.
 
mimi kama mwana ccm sina jinsi. kilichobaki ni kuhamia timu lowasa tu. kwani timu zingine zote zimepigwa double cross ya nguvu

Wacheni ujinga hiyo timu Lowasa niyachama gani.....!!
 
eti leo wanamuona Zitto shujaa,wanampamba kwa maneno yote mazuri wakati mwanzo walimtundika msalabani,wakamsulubu kwa maneno yote ya kejeli na matusi juu....leo mnauona umuhimu wake? Shame on you all......
 
naona safari ya matumaini ya bw mamvi sasa imenyooka kutoka monduli hadi magogoni. anachekeleaje!

Hahaaaaa........ "tulihuzunika pamoja tutafurahi pamoja"
Nilikua nabisha lakini sasa naamini KAJIPANGAAAA!
Sahivi anakula kahawa na pongezi nyingi from friends of Lowassa!
 
Baba Askofu,rudisha tu hela

ni kweli yametokea,ni ajali tu!!

Rudisha hela uliyopewa na Ruge

Utakua umefanya jambo la maana sana!!

HELA YENYEWE NSHAIMALIZA MWANANGU.
Ila ule mstari wa saba hauniukumu kurudisha pesa.
 
Ngoja tusubiri majibu ya profesa mhongo,hii kamati imekaa kimanjungu majungu sana.

We Jamaa ni kiaz kweli mwanzo jAna ulikuja na nyimbo Za zuio la mahamama report haitasomwa- report ishasomwa unaleta story za MWizi muhongo kesho Kuja na revenge, usichoelewa ni ninI: PAC wamechambua taarifa ya CAG na kuitolea mapendekezo kwahiyo Huyo muhongo anakuja kupinga taarifa ya CAG au mapendekezo ya PAP. KILAZA WW
 
Hawa viongozi wa Tanzania wenye mi Ph.D mbona hawaonekani kwamba hata darasa la saba wamemaliza?

Au ndiyo the ignorance or arrogance?

Juzi nimetoka kumnanga Tibaijuka hapa kwa kujaribu kutuaminisha kwamba two wrongs make a right.

Leo nasikia huyu Muhongo alisema


Sasawewe mtu ushasema fedha zina mgogoro, hujasema mgogoro umemalizwaje usharukia kuhitimisha kwamba ni fedha za IPTL?

Hizo akili kweli?

Hata kama unataka kuhadaa watu, usiidhalilishe Ph.D yako. Hadaa ki Ph.D Ph.D basi.

Sio unahadaa kama matapeli wa kila siku mitaani.
 
Hawa wenzetu hawajaanza leo tokea enzi za mwalimu tukisema wanatuambia atujasoma mara udini.Na miaka ya nyuma walikua wamezinyima uhuru media ss shemej yangu alipoingia yy kazipa uhuru ili watz wawajue wezi akina nani.
 
Nasikia huruma jamani kwa mkombozi bank...bado mbichi halafu inakutana na kashfa yote hii....
 
Mimi nahisi mjadala ndo umeisha. Kila atakayesimama atasema naachia ngazi. Hapatakuwa na michango. Tusubiri!
 
SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI. Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb) Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63 Methodius Kilaini shilingi 80.9 Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow Zitto: Bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 Zitto: Taarifa ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
 

Ingekuwa sisi wangesema sana..... hata ile MoU kati ya makanisa na Serekari ichunguzwa na Ponda aachiwe
 
eti leo wanamuona Zitto shujaa,wanampamba kwa maneno yote mazuri wakati mwanzo walimtundika msalabani,wakamsulubu kwa maneno yote ya kejeli na matusi juu....leo mnauona umuhimu wake? Shame on you all......

Tafadhali usitutoe kwenye point. Hivi unajua kama hata saa mbovu kuna wakati huonesha majira sahihi?
Akifanya mazuri apongezwe, na akifanya vibaya akosolewe pia, ndivyo binadamu anavyotakiwa kusimamiwa.
Ova
 
riport haijaficha kitu wewe unahoji kipi kipya au ndio mnataka kupoteza malengo
Sio kupoteza malengo huu ni mjadala au unataka mjadala ugeuke kuwa circlejerk?.
ripoti haijataja katika hizo pesa kiasi gani ni za umma na zipi ndo iptl walitakiwa kuchukua.hiyo maana yake cag hakufanya kazi inayotakiwa.ilitakiwa alete hesabu kwa mwenzi capacity charge wamelipa ngapi,ilitakiwa ngapi na overchanging ni ngapi,na iptl walipaswa kulipwa ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…