Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Hana shida na Triangle ya Zitto, Mkono na Mengi, anawajua vizuri sana na ndio maana alikuwa anacheka tu
yeye ni dalali wa PAP na JR,Kuwatumia Zitto,Mengi na Mkono ili kupangua ufisadi wake,ni hoja dhaifu
 
Kweli tumbili ana faida kubwa kuliko mwizi ambaye hata watalii hawawezi kuja kumwona.
 
duuuuh
 

Attachments

  • resignations.PNG
    resignations.PNG
    19.3 KB · Views: 237
mapendekezo ya PAC safi sana.
yaan nchi hii ina hela za kutisha sema wanakula wachache.
kesho tuone masultan wanajiteteaje
 
Taarifa za kuaminika toka ikulu nikuwa tayari Pinda, Tibaijuka, Mhongo na Maswa wameshawasilisha barua za kuachia madaraka na wanasubiri tu baraka za mamlaka ya uteuzi tu.

Hiyo iwe hatua ya awali kabisa. Lakini kufilisiwa na kuchukuliwa hatua ndilo liwe jambo muhimu zaidi kwa ajili ya kuweka nidhamu ya uongozi.
Ova
 
SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI. Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb) Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63 Methodius Kilaini shilingi 80.9 Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow Zitto: Bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 Zitto: Taarifa ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Duuu hawa 'watumishi' wa Mungu hawatosheki na sadaka, matoleo na fungu la moja kwa kumi hadi washadidie fedha haramu!!!
 
Samahani wadau mimi sijaona Pinda, Muhongo, Maswi, Werema, Ndulu, na Mbowe wanavyhusika. Sijaona hii report ikibainisha hela zinazopaswa kurudi.

Mwenzetu ulizaliwa kipofu...? Lkn hata kama ni hivyo basi hata masikio yamezibwa...? Lol tukuache tu
 
hapo bado hawajataja waliokula kupitia akaunti ya Harbinder Sigh Seth.
 
CCM kwa ujumla wake ni janga kwa taifa letu. Tuanze kuwatoa huku serikali za mitaa! 2015 ni kuwapiga cha mbwa mwizi.

Na MKOMBOZI Bank ni MAGUMASHI. Wanauza hisa ili kutakatisha uwekezaji wa hao wezi na mafisadi akiwemo Kilaini na Nzigirwa. Na itakufa wakifilisiwa...
 
PAC chini ya uongozi wa Zitto, imefanya kazi nzuri sana na ya kijasiri kuhusiana na suala hili......

Lakini suala la utovu wake wa nidhamu na usaliti kwa CDM ni jambo lingine ambalo linaangaliwa kwa merits zake. Alijiona yeye ni zaidi ya Chama na kwa tabia zake ambazo mimi binafsi nime-muobserve tangu 2009 naamini hatabadilika !

Hafai kabisa kurudishwa CDM !.....Simply hafai !. Aende akaendeleze chama chake cha ACT alichokianzisha na Kitila !

Wakari tunaelekea 2015 chadema itafakari namna ya kuziba mianya yote inayoweza kuikosesha kura hâta moja wakati wa uchaguzi wa 2015. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na Zitto kurudishwa kundini kwa garama yoyote. Kwa muonekano wa dhahiri zitto ni mwana cdm halisi anayeipenda cdm kwa moyo wake wote. Zitto amejifunza na chadema imejifunza kitu Pia kutokana na yaliyototokea ndani ya cdm. Kwenye mkakati huo CUF imrudishe Hamadi Rashid Pia ili kulinda kura za hamadi na zitto zisipotee kwenye UKAWA. Kufanya hivyo ni sehemu ya mpango mkakati wa kukamata dola 2015. Nikimuangalia zitto ataisaidia sana cdm mbele ya safari. Chama kitumie its uncommon sensé kufanya uwamuzi huu mzito wa kikomavu
 
Jina limemkaa Aliyekuwa jaji Werema na aliyekuwa AG. Tumbili kakamata mwizi.
 
NIlivyotazama uchambuzi, inawezekana huyu Muhongo kilichomponza ni U-much know wake. Ni mtu mwenye kiherehere cha kuonekana anajua kuliko wengine. Hivyo kila mpiga dili akataa akutane naye ofisini kwake, kwa picha na waandishi wa habari.

Sasa hili limekuja kuwa kitanzi chake,kwa kuwa dalali. Hili sio kosa kubwa sana KAMA angekuwa mstaarabu na angeweza kumiliki domo lake chafu vizuri.

ANgekaa kimya, angeweza ku-come out of this. Hapa ndio utaona Busara za Mk.were, ingawa akili za darasani nusu kijiko, ila busara za pwani zinamsaidia kupisha upepeo.

Kijamaa kimekaa kimya utafikiri kilikuwa hakijui kilichokuwa kinaendelea, na inawezekana kilishiriki. lakini utaanzia wapi sasa kumuunganisha?

Hapa wenye midomo mirefu, midomo imewahukumu, kuanzia Muhongo, maswi, Werema hadi Pinda.

Ni wakati muafaka Chenge akajiuzulu kule kwenye KATIBA pia.
 
Back
Top Bottom