Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI.

Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)

Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.

Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.

Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4

Soma pia: Uzi maalum wenye matukio yote yaliyojiri kwenye sakata la ufisadi wa ESCROW

Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.

Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.

Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.

Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9

Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.

Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow

Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006

Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.

Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
 
Asante JF kwa kutuhabarisha, Hongereni kamati ya PAC mapendekezo yenu. Kama mapendekezo yale yatatekelezwa kwa asilimia mia moja....Tanzania inaweza kurudi kwenye mstari ulionyooka na kujiendesha bila tatizo.
 
Naongelea uwasilishaji, si huo uchunguzi. Na pia tumesikia upande mmoja mpaka tungoje upande wa pili wanasemaje.

Mpaka sasa sijaona kilichowasilishwa ambacho hakijibiki.

Hahahahahaaaaa upo? Nakukumbuka sana ulivyokua Unakataaa na kuutetea huu wizi. Kazi unayo, maana suala sio kujibika suala ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu.
 

Attachments

  • 1417021127620.jpg
    49 KB · Views: 234

Unaposema Mkombozi wametakatisha fedha huoni kama na benki kuu nao wanahusika katika utakatishaji huo?
 
Mim nalia na viongozi wa dini "toa ndugu toa ndugu ulichonacho mungu anakuona mpaka moyoni mwako" ,sasa kweli amewaona ,vipi mlitoa fungu la kumi? Kwa hizo fedha za madafu mlizogawana kwenye viloba ,nchi hii itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno makubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 


We kilaza umeambiwa mchakato mzima ni tapeli mtupu,documents Za kufoji etc. Pap/iptl haikutakiwa kulipwa chochote Kabla ya uamuzi wa court ya kimataifa iliyoshugulikia mgogoro huo.
 


1.6B pesa kuchu sana mamaa, hukumsikia Chenge aliziita vijisenti? nadhani za RICHMONDI zilishaisha hivyo akahitaji kujiboost kidogo.

Hayo magorofa huko mbezi beach, ma-vogue hapo mtaani unafikiri yananunuliwa na mishahara?

mshahara wa waziri inabidi asiule miaka si chini ya mi 3 ili kulipia vogue moja tu hapo CMC.

Sasa kwa akili yakako unafikiria wananunua kwa kutumia nini?miradi ya kuku? WIZI.
 
Jina limemkaa Aliyekuwa jaji Werema na aliyekuwa AG. Tumbili kakamata mwizi.
hahahaaaa!! kuna siku mgimwa alisema itabidi tumbili ajulikane ni nani, na mwizi ni nani!!
 
aibu mahakama kuu kuweka katazo kuzuia kashfa
ya kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa zaidi ya
mabilioni kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow.
 
Pope John Paulresigned with nothing,hakuwa hata na kijiko..now look at Religious Thug..shame on you au ndo Freemason?

Pope John Paul ii DIDN'T resign, Pope Benedict xvi DID. You've got a good point though, our leaders are too selfish nowadays!
 
Habinder Singh seth wewe Ni kiboko umeangusha serikali tena Kama ulivyoangusha Kenya. Wewe Ni level za kimataifa.
 
Nimesoma ripoti yote, pamoja na uzuri wake sijaona mahali kilipojumuishwa kielelezo cha utetezi wa BoT ambacho kiligusia uhusika wa ofisi kuu
Anyway angalao kuna debate kuhusu hizo pesa!
 
Mkombozi bank walikuwa wanajua hizi ni fedha za deal; no question about it. Stanbic bank walikuwa wanajua hizi ni fedha za deal, no question about it. Ila walijua na pengine wameshagawa fedha kwa mtindo huo mara nyingi, kuwa hakuna sheria yoyote itakayofanya kazi. Tatizo la nchi yetu si kutunga sheria nyingi zaidi na kuongeza vyombo vya utekelezajia. Tatizo letu ni kuwa taasisi ambazo zinatakiwa kuzitumia sheria hawazitumii na hivyo inaonekana kama vile hazitoshi. Tatizo liko kwenye enforcement ya sheria. Waziri mkuu kila siku ilikuwa ni kudanganya kuwa hiyo ni hela ya binafsi akijua wazi kuwa si kweli. Na aende tuuuuu!! Useless.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…