Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Labda nikupe mfano halisi. Kuna mama alitaka kuniuzia kiwanja kwa hati ya mauziano ya serikali ya mtaa. Siku ya mauziano pale serikali ya mtaa nikadai ofa ile hati ya umiliki, mama akasema hati ya umiliki hana bali anayo hati ya mauziano baina yake na yule wa muuzaji wa awali na ameishi pale zaidi ya miaka 12 wala hakuwahi kubughudhiwa na serikali ikakiri kumtambua. Hati ya umiliki nikapewa jibu kuwa aliipoteza kwenye mafuriko ya jangwani.

Maelezo yake yakanipumbaza nikafanya malipo na kupewa hati ya mauziano ya serikali ya mtaa mbele ya mwenyekiti na ile ya awali waliouziana na mmiliki wa kwanza.

Kizaazaa kilikuja pale nilipoenda wizarani kuangalia namba ya kiwanja mmiliki wake ni nani. Nilikuta jina la mtu mwingine tofauti kabisa na haya majina mawili ya wamiliki waliotangulia. Kuna mtu toka 1996 ameandikwa ardhi kama mmiliki na huyo ndo anatambulika kama mwenye hati miliki. Kwahiyo huo ndo ulikua mwanzo wa kujua kama nilipigwa changa la macho.. na wale wamama mpaka leo wanajitetea kuwa ile ilikuwa ni sehemu yao ya halali. kibaya zaidi huyo anayesomeka wizarani kama mmiliki kila ninakouliza kuanzia wale wamama, serikali za mtaa na majirani kila mtu anadai kutokumfahamu huyo mtu na wala hawajawahi kumuona. Kwa maana hiyo inawezekana alijimilikisha kiwanja kile kwa njia zisizo sahihi lakini mkienda kwenye sheria yeye ndo atatambulika kama mmiliki halali kwani ndo mwenye hati miliki. Mpaka leo nimeogopa kujenga pale zaidi ya kuacha kajumba kadogo nilikonunuliana na kiwanja chake.

KUWA NA HATI YA MAUZIANO SHERIA HAIKUTAMBUI KAMA MMILIKI HALALI. HATI MILIKI NDIO KILA KITU.

Hapo ndio singasinga kapigwa changa la macho na Iptl. Labda nikuibie siri ya kufikirika. Inawezekana hati miliki mpaka sasa inamilikiwa na bank iptl alikochukua mkopo.

Huyo rafiki wa masingasinga (faizafoxy)hawezi kuja kujibu chochote!! Ila pia usishangae IPTL na PAP ni huyohuyo na kilichofanyika ni kiini macho tu!!
 
Huyo rafiki wa masingasinga (faizafoxy)hawezi kuja kujibu chochote!! Ila pia usishangae IPTL na PAP ni huyohuyo na kilichofanyika ni kiini macho tu!!

Na kama sijasikia vibaya hiyo ripoti ya zitto iligusia kidogo juu ya hili jambo kuwa walipofanya uchunguzi wakagundua kuwa Iptl ndo huyohuyo PaP.

Kwa maana hiyo sisi kama wapiga ramli tunaweza kubashiri kwamba toka zamani mikataba inaingiwa Singasinga ndo alikua mmiliki wa Iptl. Amechukua mkopo Bank kuendeshea mradi. Akataka kuitapeli Bank kwa kuifilisi Iptl na tena kuja kuinunua Iptl kupitia kampuni mpya ya PAP. Tatizo likaja kwenye hati miliki kwani ukichukua mkopo bank kwa niaba ya kampuni yako lazima uwakabidhi hati miliki ya mradi wako kama dhamana. Hii inafanyika hata huku mitaani kwetu.

Ukienda NmB kuchukua mkopo wa biashara ndogondogo mfano milion 5 ni lazma uache hati miliki ya mali isiyohamishika eidha nyumba au kiwanja. Na siku ukifilisika Bank mwenye hati miliki uliyoweka kama dhamana kule ndio anatambulika kama mmiliki wa ile mali.

Lakini kwenye miradi mikubwa ya makampuni kama haya ukichukua mkopo bank huwapi dhamana mali zako bali unawapa dhamana ya hati miliki ya mradi wa kampuni itakayojengwa.

Na kwakuwa makampuni makubwa yote sharti yawe Bima bwana seth singasinga alitumia mwanya huo kuitapeli Bank kwa kuifanya iptl imefilisika akitarajia Bank wataidai Bima alafu yeye arudi kwa picha nyingine ya PAP kama mnunuzi wa kampuni iliyofilisika ili aruke kihunzi cha kulipa mkopo. Bahati mbaya hela ya Mzungu hailiki kifalafala. Bank wakafungua kesi kudai uhalali wa kumiliki mtambo kwani ndio wenye hati miliki. Hapo ndo msingi mkuu wa tatizo lote lilipo.
 
yeye ni dalali wa PAP na JR,Kuwatumia Zitto,Mengi na Mkono ili kupangua ufisadi wake,ni hoja dhaifu

Dada Victoire, Triangle inaanza kujionyesha Polepole,

take your time, jiachie akili zako uwe huru kisha pitia report zote, ya PAC na hiyo ya Muhongo
 
Last edited by a moderator:
By OLesendeka: haitaji kuwa na elimu kubwa kujua kama hapa hakuna uarifu na kusema report ni fake ila inahitaji kuwa na faili la mirembe tu kukataa report ya C.A.G na kukataa report ya PaC.. Plz sio mm niliyesema.
 
wadau wa JF naomba kusaidiwa majibu ya maswali yanayonitatiza mpaka sasa

1. Kama Rugemarila(VIP) amemuuzia Singasinga(PAP) 30%, je mmiliki wa 70% ni nani na ni kweli naye ameuza hisa zake?

2. Kama huyo mmliki wa 70% hajauza hisa zake mbona hajajitokeza kuukana umilikiwa PAP wa kampuni yake na fedha zake!?

4. Je huyo wa 70% akijitokeza leo atalipwa vipi sehemu yaESCROW
3. Kutojitokeza kwa mmliki wa 70% kukanusha mauzo je, hakumaanishi kuwa ndiyo huyohuyo aliyejigeuza kuwa PAP na kumnunua(buy out) VIP?
 
Kwa mujibu wa ripoti ya PAC mmiliki wa 70% alikuwa Mechmar baadaye ukafanyika ujanja ujanja umiliki ukahamia Piper Link kimagumashi kisha kutua kwa PAP.
 
spika makinda alisema wengine hapa mnapiga kelele nikiwaamsha hata hamjui cha kusema hili ni fumbo la imani kuna IPTL,PAP,MECHMAR, VIP,PIPERLINK,SIMBA TRUST ,STANDARD CHATTERD HONGKONG SIJUI MALAYSIA ,MKONO ADVOCATE,zote hizo ni wakala wa shetani
 
wadau wa JF naomba kusaidiwa majibu ya maswali yanayonitatiza mpaka sasa

1. Kama Rugemarila(VIP) amemuuzia Singasinga(PAP) 30%, je mmiliki wa 70% ni nani na ni kweli naye ameuza hisa zake?

2. Kama huyo mmliki wa 70% hajauza hisa zake mbona hajajitokeza kuukana umilikiwa PAP wa kampuni yake na fedha zake!?

4. Je huyo wa 70% akijitokeza leo atalipwa vipi sehemu yaESCROW
3. Kutojitokeza kwa mmliki wa 70% kukanusha mauzo je, hakumaanishi kuwa ndiyo huyohuyo aliyejigeuza kuwa PAP na kumnunua(buy out) VIP?
Mmiliki wa 70% ni Standard Chartered Bank Hong kong, na Tanzania lazima itakuja kumlipa.
 
Back
Top Bottom