Kumekucha jamani, tamthiliya ya eskroo Ni episodi nyingine Leo, lakini Kuna jambo tofauti nafikria, sawa Zito na Deo wanastahili kupongezwa kwa niaba ya kamati ya PAC!, Lakini mbona sifa zinazidi kwao Tu wakati Wao Ni waleta chakula(kitoweo) mezani. Mbona muwindaji mahiri kwenye pori hatari(Kafurira a.k.a kaka WA taifa) tunamsahau!?.
Jamani kakoswakoswa na Na mengi huyu.
Jamani katukanwa Sana huyu(tumbili).
Jamani taifa zima lilikuwa linaimba katiba mpya, lkn yeye aliamua kufikria nje ya box.
Jamani kawpiga knock out watu wenye mamlaka ya kidola kwenye lips í-½í±„ zao,
Sasa linapokuja suala la sifa mbona tunaishia kuwasifu wahudumu wa mezani kwa utumishi uliotukuka lakini muwindaji/mpishi tunamchukulia poa!?.
Jamani mwenzenu hili linanikereketa.
Tutende haki kwa kaka WA Taifa. Nawasilisha.