Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakati watanzania wameaminishwa kuwa hela ya Tegeta Escrow Account ni za serikali,wajanja wachache wachota mabilioni ya shilingi za kitanzania kiulaini.
Taarifa zilizovuja kutoka vyanzo vya uhakika vinaelezea kuwa uhusiano wa Singh na washirika wa Lowassa ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi wa nchi jirani ambayo ni mwanachama wa EAC.
Baada ya uchaguzi huo kumalizika na kundi hilo kushindwa walihamia Tanzania ambapo mpango mahususi wa wizi wa hela halali za Benki moja iliyopo Far East Asia ulifanywa.
Mchezo huu ulichezwa kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo nyaraka za kughushi ziliandaliwa na kundi hili ili kuhalalisha wizi huu uliowapa faida ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.
Benki moja nchini ilitumika kupitisha hela hizo,Meneja wa benki hiyo na baadhi ya wafanyakazi wengine wenye uhusiano wa karibu sana na Lowassa wameshafukuzwa kazi.Meneja wa Benki hii ni raia wa nchi jirani mwanachama wa EAC na yupo katika timu ya kampeni ya Lowassa.Meneja huyu ndio aliruhusu hela zitolewe taslimu na kwa kiasi kikubwa sana.
Baada ya kuona wao wameshachafuka,Lowassa na mshirika wake mkubwa katika biashara mwenye asili ya kiasia,walimkabidhi mfanyabiashara mmoja wa kiasia kazi ya kuwa na mtuhumiwa huyo.
Kazi kubwa waliyoifanya ni pamoja na kuwaaminisha watanzania kupitia vyombo vya habari wanavyovimiliki kuwa fedha zile ni mali ya umma na hivyo kuondoa nafasi ya wananchi kuwasogeza karibu na wizi huu.
Walitengeneza mazingira ya kila hila kuonesha kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikalini wameshiriki kuiba na kula fedha hizo.
Hoja iliyowasilishwa bungeni ilikuwa ni wizi wa fedha za umma,lakini mwisho wa mjadala huo ambao ulipamba moto sana,uliishia kutoa adhabu kwa watendaji wa serikali kuwa walikuwa wazembe na waziri mmoja kushitakiwa kwa kusema uongo bungeni jambo ambalo ni tofauti kabisa na hoja ya msingi ilipowasilishwa.
Alikuwepo na alijua vema kinachoendeleaHivi Magufuli alikuwa sehemu ya hiyo serikali? Nauliza tu...!
Kwa miaka kama ishirini serikalini kama waziri kama sikosei kwa hiyo anajua kinachoendelea.Hivi Magufuli alikuwa sehemu ya hiyo serikali? Nauliza tu...!
Chenge ni wakati wake akatubu na kurudisha hizo pesa
Naamini kuwa serikali inamwogopa Chenge. Huyu Chenge a.k.a nyoka wa makengeza alipiga hela za rada akaficha visiwa vya new jersy hata serikali ilipojua ikagwaya. Kapiga za Escrow hata akatangaza kuwa bil.1.6 ni vijisent tu bado serikali imegwaya. Hata kwenye upelelezi hayumo. Namwomba namba moja amsweke ndani au awaachie wote walioko mahabusu.Dhulumati na roho mbaya shetani anayesingizia watu makosa na kuwaacha wahusika huu uzi unakila kitu alaaniwe yeye na kizazi chake anayewaonea wasiohusika huku akiwajua wahusika vizuri kabisa.