Labda nikupe mfano halisi. Kuna mama alitaka kuniuzia kiwanja kwa hati ya mauziano ya serikali ya mtaa. Siku ya mauziano pale serikali ya mtaa nikadai ofa ile hati ya umiliki, mama akasema hati ya umiliki hana bali anayo hati ya mauziano baina yake na yule wa muuzaji wa awali na ameishi pale zaidi ya miaka 12 wala hakuwahi kubughudhiwa na serikali ikakiri kumtambua. Hati ya umiliki nikapewa jibu kuwa aliipoteza kwenye mafuriko ya jangwani.
Maelezo yake yakanipumbaza nikafanya malipo na kupewa hati ya mauziano ya serikali ya mtaa mbele ya mwenyekiti na ile ya awali waliouziana na mmiliki wa kwanza.
Kizaazaa kilikuja pale nilipoenda wizarani kuangalia namba ya kiwanja mmiliki wake ni nani. Nilikuta jina la mtu mwingine tofauti kabisa na haya majina mawili ya wamiliki waliotangulia. Kuna mtu toka 1996 ameandikwa ardhi kama mmiliki na huyo ndo anatambulika kama mwenye hati miliki. Kwahiyo huo ndo ulikua mwanzo wa kujua kama nilipigwa changa la macho.. na wale wamama mpaka leo wanajitetea kuwa ile ilikuwa ni sehemu yao ya halali. kibaya zaidi huyo anayesomeka wizarani kama mmiliki kila ninakouliza kuanzia wale wamama, serikali za mtaa na majirani kila mtu anadai kutokumfahamu huyo mtu na wala hawajawahi kumuona. Kwa maana hiyo inawezekana alijimilikisha kiwanja kile kwa njia zisizo sahihi lakini mkienda kwenye sheria yeye ndo atatambulika kama mmiliki halali kwani ndo mwenye hati miliki. Mpaka leo nimeogopa kujenga pale zaidi ya kuacha kajumba kadogo nilikonunuliana na kiwanja chake.
KUWA NA HATI YA MAUZIANO SHERIA HAIKUTAMBUI KAMA MMILIKI HALALI. HATI MILIKI NDIO KILA KITU.
Hapo ndio singasinga kapigwa changa la macho na Iptl. Labda nikuibie siri ya kufikirika. Inawezekana hati miliki mpaka sasa inamilikiwa na bank iptl alikochukua mkopo.