Wakati watanzania wameaminishwa kuwa hela ya Tegeta Escrow Account ni za serikali,wajanja wachache wachota mabilioni ya shilingi za kitanzania kiulaini.
Taarifa zilizovuja kutoka vyanzo vya uhakika vinaelezea kuwa uhusiano wa Singh na washirika wa Lowassa ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi wa nchi jirani ambayo ni mwanachama wa EAC.
Baada ya uchaguzi huo kumalizika na kundi hilo kushindwa walihamia Tanzania ambapo mpango mahususi wa wizi wa hela halali za Benki moja iliyopo Far East Asia ulifanywa.
Mchezo huu ulichezwa kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo nyaraka za kughushi ziliandaliwa na kundi hili ili kuhalalisha wizi huu uliowapa faida ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.
Benki moja nchini ilitumika kupitisha hela hizo,Meneja wa benki hiyo na baadhi ya wafanyakazi wengine wenye uhusiano wa karibu sana na Lowassa wameshafukuzwa kazi.Meneja wa Benki hii ni raia wa nchi jirani mwanachama wa EAC na yupo katika timu ya kampeni ya Lowassa.Meneja huyu ndio aliruhusu hela zitolewe taslimu na kwa kiasi kikubwa sana.
Baada ya kuona wao wameshachafuka,Lowassa na mshirika wake mkubwa katika biashara mwenye asili ya kiasia,walimkabidhi mfanyabiashara mmoja wa kiasia kazi ya kuwa na mtuhumiwa huyo.
Kazi kubwa waliyoifanya ni pamoja na kuwaaminisha watanzania kupitia vyombo vya habari wanavyovimiliki kuwa fedha zile ni mali ya umma na hivyo kuondoa nafasi ya wananchi kuwasogeza karibu na wizi huu.
Walitengeneza mazingira ya kila hila kuonesha kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikalini wameshiriki kuiba na kula fedha hizo.
Hoja iliyowasilishwa bungeni ilikuwa ni wizi wa fedha za umma,lakini mwisho wa mjadala huo ambao ulipamba moto sana,uliishia kutoa adhabu kwa watendaji wa serikali kuwa walikuwa wazembe na waziri mmoja kushitakiwa kwa kusema uongo bungeni jambo ambalo ni tofauti kabisa na hoja ya msingi ilipowasilishwa.