Full Time: Azam FC 1 - 2 Young Africans SC | NBC Premier League | Azam Complex | 10-04-2025

Tembosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
5,037
Reaction score
4,932
SIKU YA MECHI KALI.

1000051682.jpg

🏆 #NBCPremierLeague
⚽️ Azam Fc 🆚 Young Africans SC
📆 10.04.2025
🏟 Azam Complex
🕖 1:00 Jioni

VIKOSI VINAVYOANZA LEO.
1000051973.jpg

1000051969.jpg

Updates....

Dakika 11 Pacome anaipatia goli la kuongoza kwa Yanga

Dakika 19 Pacome anatolewa nje kupata matibabu zaidi baada ya kuumizwa

Dakika 34, Dube anafunga goli la pili kwa Yanga.

1000052046.jpg

2ND HALF.
Updates
1000052120.jpg
 
Huh.. twende tukampige lambalamba asilete mazoea kwenye mambo serious. Najua kolo anaifatilia hii mechi akitegemea atafaidika kwa chochote. Pole sana bi mkubwa leo ni zamu ya bi mdogo
 
Attachments

  • Screenshot_20250410_024655_Instagram.jpg
    Screenshot_20250410_024655_Instagram.jpg
    505.7 KB · Views: 54
  • 1743762882825.jpg
    1743762882825.jpg
    377.6 KB · Views: 57
Nimesikia msemaji wa Simba amelia kwa firaha baadaya kufuzu nusu fainal ya kombe la kina Mama
Sasa najiuliza siku Simba wakifika fainal kama Yanga hali itakuaje!!

Namuona Mangungu akimwaga Machozi ya kutosha., Kwa hakika Yanga ni kipimo cha Soka la Kimataifa jwa apa Tanzania.
 
Na Mimi nimeshangaa mtu mzima analia eti kwa kuwatoa waarabu wa igunga kwa penalty kaona ni jambo ambalo ni la ajabu sana kwake🤣🤣
Wenzake wamekipiga fainali na kushinda uko uko ugenini wangekuwa wao angezimia na kufa kabisa maskini!
 
Mwanaume kulia lia hovyo na yenyewe haijakaa poa hata kidogo. Yaani timu kuingia nusu fainali, tena kombe lenyewe ni la shirikisho! Ndiyo umwage machozi!!
 
Na Mimi nimeshangaa mtu mzima analia eti kwa kuwatoa waarabu wa igunga kwa penalty kaona ni jambo ambalo ni la ajabu sana kwake🤣🤣
Wenzake wamekipiga fainali na kushinda uko uko ugenini wangekuwa wao angezimia na kufa kabisa maskini!
ile timu sasahivi ipo majnuni!, so kufuzu pale ilikuwa ni kama muujiza!
 
Nimesikia msemaji wa Simba amelia kwa firaha baadaya kufuzu nusu fainal ya kombe la kina Mama
Sasa najiuliza siku Simba wakifika fainal kama Yanga hali itakuaje!!

Namuona Mangungu akimwaga Machozi ya kutosha., Kwa hakika Yanga ni kipimo cha Soka la Kimataifa jwa apa Tanzania.

Na Mimi nimeshangaa mtu mzima analia eti kwa kuwatoa waarabu wa igunga kwa penalty kaona ni jambo ambalo ni la ajabu sana kwake🤣🤣
Wenzake wamekipiga fainali na kushinda uko uko ugenini wangekuwa wao angezimia na kufa kabisa maskini!

Mangungu akiona hiki ulichoandika hapa, lazima amwage machozi ya kutosha na kujiambia mwenyewe "hapa kweli kijana ninaye"
Hebu acheni kujitoa ufahamu ninyi wenyewe mlifika fainali kwa kukutana na vibonde kina Rivers na Marumo kwenye hatua za robo na nusu, hao waarabu wanacheza ligi ya Misri na wako nafasi ya nne siyo wale wenu wa Algeria ambao mlishindwa kuwafunga japo goli moja tu la kuwafanya mfuzu, halafu niwakumbushe tu wale vibonde wenzenu mliokuwa nao kundi moja huko wote wameishia robo huku Simba na mwenzie Constantine wote wako nusu
 
Usifananishe vitu wewe,,kikombe cha kahawa usiwe unalinganisha na waliokuwa kwenye ligi ya wanaume,,Pengine ubora wa Al masry umeuona wewe peke yako kwamba ni timu Bora ya kuifunga mpaka ukalia🤔🤔
 
Hebu acheni kujitoa ufahamu ninyi wenyewe mlifika fainali kwa kukutana na vibonde kina Rivers na Marumo kwenye hatua za robo na nusu, hao waarabu wanacheza ligi ya Misri na wako nafasi ya nne siyo wale wenu wa Algeria ambao mlishindwa kuwafunga japo goli moja tu la kuwafanya mfuzu, halafu niwakumbushe tu wale vibonde wenzenu mliokuwa nao kundi moja huko wote wameishia robo huku Simba na mwenzie Constantine wote wako nusu
Kijana wa Mangungu! Mbona umeni quote bila ya sababu?
 
Back
Top Bottom