Ngoja niwaelekeze Hawa wajinga wasiojua maana ya Derby ,, Derby kwenye mpira Ni upinzani mkali baina ya timu mbili katika eneno , ukanda, au nchi, au bara, huwezi kuzungumza Derby bila upinzani /uhasama wa Hali ya juu. Derby inaweza kusababishiwa na vitu mbalimbali Kama wachezaji, viongozi, eneo, wawekezaji n.k mfano Derby ya Manchester United Vs Liverpool ambayo ndio derby kubwa uingereza ilikuzwa Sana na wachezaji Gigs na Gerald. Derby ya Spain inayohusisha Timu kutoka Catalonia na Spain (Real Madrid) ilidabaishwa na Vita au kwa ufupi tunaweza kusema Siasa , vile vile upinzani wa Messi na Ronaldo uliifanya Derby hii inayoitwa El clasico kuwa Derby Bora zaidi ulimwenguni. Hata dini zinatengeneza Derby mfano
Celtic (Catholic) and Rangers (Protestants)
Zipo
pia Derby za mataifa mfano Poland Vs Germany , Uganda Vs Tanzania ,, kwahiyo kila Derby Ina chimbuko lake na vitu vinavyoikuza, pia Derby huweza kufa au kupoteza mvuto.