Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Tokea ziongezwe zile dakika 7 hakuna mchezaji yeyote aliyedondoka chini mpira muda wote ulikuwa unachezwa. Refa ameibetia Simba
Kata rufaa Utopolo. PELEKA malalamiko TFF.Hayo ni maagizo ya FIFA kwa marefaa kwamba waongeze dakika kwa timu zinazopoteza muda kwa makusudi.Ndio maana Uingereza sio ajabu kuona mpira unaongezwa dakika 12.
 
Wanaolalamika Kwamba Dakika za Nyongeza Ndo zimefanya Simba wapate goal..
Wanasahau kuwa Dakika Ziliongezwa Kwa Wote Waarabu na Simba..
Kwani dakika Zilipoongezwa Waarabu walifungwa Miguu?

Vipi kama Waarbu wangetushenyenta Goal Mngesema Kuwa Dakika zimeongezwa..
Punguzeni Wivu unawafanya Msiendelee Na majungu..

Halafu Nilisahau Hivi mtani Unapoint Ngapi Kweli?

Na Umeshika nafasi ya Ngapi kwenye Group lako??
 
Nidhamu ya waarabu imewaponza, toka awali walikuwa wanacheza kwa mbinu zao za kujiangusha mara waingize mipira miwili miwili na nafikiri walimjibu refa vibaya!, nashuku walimtukana sasa nayeye akaamua atumie mamlaka yake!.
kuongeza dakika 7 haikuwa shida ila kwenye nyongeza kaongeza zikafika 9, na ubovu goli limepatikana ktk dakika ambazo hazikuwa zile saba!.

Naweza sema refa kaishi usemi wa simba yani "Ubaya ubwela!"...🤣

Oni langu..
Ni muda sasa timu za kaskazini haswa waarabu wabadilishe nidhamu za uchezaji wao, figisu figisu za ajabu zitakuwa zinaleta tafrani kwa wapinzani na hata refa kama ilivyojitokeza hivi leo.
CAF wamekuwa wakiwalea hawa waarabu nafikiri waongee nao.
 
We mwarabu Koko. Refa kachezesha vizuri. Hayo maarabu yanatuoneaga kila siku. 😀😀😀😀
Hakuna uzuri wowote kaonesha wazi wazi kuwa kaibetia Simba. Mchezaji wa CS Sfaxien alikuwa kachezewa faulo na Melon lakini alifanikiwa kuwin mpira na alikuwa anaenda kufunga kwanini hakuacha advantage pale badala yake kaona Che Melon kaachwa kapuliza kipyenga cha faulo na kumpa che Melon kadi ya njano wakati alikuwa ni mtu wa mwisho aliyezuia goli kufungwa.

Kaongeza dakika 7 bado haitoshi, hakuna tukio lolote la mpira kusimama kwenye hizo dakika lakini hakuridhika mpaka aone Simba inapata goli ili mkeka utiki
 
Refa kashinda. FIFA na CAF waiangalie hii issue ya marefa kutokuheshimu muda halali wa mchezo na kuamua wanavyoona wao vinginevyo uhuru wa marefa unaweza kusababisha malalamiko kwa timu ambazo zinafungwa baada ya muda rasmi wa nyongeza kuisha.
Ungekuwa na akili ungeona upumbavu wa hizi timu za kiarabu zinavyopoteza muda bila sababu za msingi. Uliona wapi ulaya timu zikipoteza muda kifala kama timu zetu hizi za kiarabu?
 
Wanaacha kukubali na matokeo wao wanaleta fujo

Huyu Kibu aliwafunga Tripoli iliyokuwa na mchezaji wa bilioni 5 tena kwa akrobatiki lakini waarabu wale walitulia tu.

Sasa wao header mbili tu tayari wameanza kuleta fujo kwa kocha.

Mechi ijayo Kibu tutakuwa hatumpangi sasa.
Badala ya kucheza wenyewe wanasubiri refa apulize filimbi , wamepata walichokitaka wasitafute wa kumlaumu
 

1734276296110.jpeg
 
Back
Top Bottom