Full Time: Simba SC 3-0 Tanzania Prisons | NBC Premier League | KMC Complex | 11 Februari, 2025

Full Time: Simba SC 3-0 Tanzania Prisons | NBC Premier League | KMC Complex | 11 Februari, 2025

Sijui kwa nin hatufungi magoli mengi sec half. Wachezaj waambiwe hizi timu za kufunga hata 7 zipigwe tu.
Kila mchazaji huwa anataka kufunga...hakuna struker mwenye utulivu by nature...natamani kuona combinations ya MPANZU na striker mwingine mwenye utulivu...
 
Hii kawaida ya simba kuridhika na matokeo haifurahishi.. hii ilikua nafasi kwao kuongeza GD. Sub zote hakuna iliyofanya kazi. Wanacheza "Relaxation football"
Hapa ni mtizamo wa kocha na wachezaji wanarithishana hii tabia.

Wao wakifungwa sawa na wakifunga poa tu. Hii ndiyo tabia ya wachezaji wa Simba miaka yote.

Yanga wakipata goli tatu wanataka wapate nyingine tatu... Hii nayo ni tabia ya utopolo miaka nenda miaka rudi.
 
Simba wapo ivo tangu enzi za Sunderland na Yanga ni watu wa jihadi hata kabla ya Tabu Mangara hajaanzisha Pan Africa!
Tunakwama hapa kila siku. Hapa siongelei mpira wa nguvu au jihadi, naongelea kupoteza nafasi za wazi. Ukiangalia hata kimataifa tunakwama kila msimu kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi hasa uwanja wa nyumbani. Tusilee tatizo kwa kusema ndiyo kawaida yetu.

Tunawazodoa Yanga kwa kuzifunga timu goli 5 na 6 ila kuna mechi hata Simba ina uwezo wa kushinda goli hizo ila mapuuza yanakuwa mengi.
 
Timu vibonde kama hizi yanga uwa anatoa dozi ipasavyo kuanzia chuma 5+,,kushinda 5 au 6 sio kwa Kila timu!
 
Back
Top Bottom