FULL TIME: Simba Sc 4-1 AS Vita | CAFCL | Mkapa Stadium

FULL TIME: Simba Sc 4-1 AS Vita | CAFCL | Mkapa Stadium

Pununkila

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2021
Posts
689
Reaction score
1,706
00' Mwamuzi anapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mchezo

30' Luis Miquissone anapiga goli la kwanza kwa upande wa Simba

32' Goli la Simba halidumu baada ya Zemanja Soze wa AS Vita kusawazisha dakika mbili baada ya goli la kuongoza la Simba

45+1' Cloutas Chama anaifanya Simba kumaliza kipindi cha kwanza vizuri baada ya kuiongezea Simba bao la pili

45+2' Mapumziko

66' Larry Bwalya anaweka goli la tatu kwa shuti kali, Simba 3-1 AS Vita

84' Cloutas Chama anakandamiza bao la nne

90' Mpira umekwisha na Simba inakusanya alama 13 ambazo hazitaweza kufikiwa na yeyote kundi A bila kujali matokeo ya mechi za mwisho


==========

Kikosi kinachoanza Leo dhidi ya as Vita club

FB_IMG_16174514631420374.jpg


 
Morson leo anasafisha nyota ya ushindi.
Kila la kheri mnyama
 
Ila huyu Mugalu atakuwa ana limbwata sio bure....yaani anasifiwa sana halafu uwanjani ni low class striker....

Anapangwa kila mechi....itakuwa anatumia vumbi la Congo.
Jamaa anakitu fulani ivi cha kipekeee kinachomfanya awe juu ya wenzake.


Wengi mnawaza kufunga tu magoli.


Mugalu anaficha mpira, mtu ambaye akiwa na mpira unaona mashambulizi yanavyopangwa , ana kaba vzuri

Mie sio mchambuz wa mpira[emoji23][emoji23]
 
Bora wewe umeiweka vizuri heading

Leo naiona droo, sina hakika ya ushindi kwa timu zote
 
Ila huyu Mugalu atakuwa ana limbwata sio bure....yaani anasifiwa sana halafu uwanjani ni low class striker....

Anapangwa kila mechi....itakuwa anatumia vumbi la Congo.
Mugalu ni mzuri kwenye kumiliki mpira..na second ball..
Kumbuka mechi hizi Ni vizuri mtoke hata bila goli lakini msifungwe..akina boko na MK wanaweza kufunga lakini tukizidiwa tukapaki basi wakabaki peke yao mbele..wanakuwa vituko..yaani sio wazuri wakibaki peke yao.
 
Swali linajieleza hapo juu
Kwa tulio mbali na Azam Nani mwingine anaonesha mechi ya Simba na Vita leo!
 
Back
Top Bottom