Full Time: Tanzania 2-0 Burkina Faso | Mechi ya ufunguzi CHAN | Mkapa Stadium | Agosti 2, 2025 | Saa 2 Usiku

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu!

Leo Agosti 2, 2025 pazia linafunguliwa rasmi kwa Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024, ambapo Tanzania itavaana na Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Michuano ya CHAN 2024 inafanyika katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Je, Taifa Stars kuibeba mabegani Tanzania?

Updates

Mwamuzi atakaesimamia mchezo wa kwanza wa fainali za michuano ya CHAN 2024 kati ya Tanzania dhidi ya Burkina Faso ni Loutfi Bekouassa kutika Algeria.

​
Mwamuzi huyo atasaidiwa na Adel Abane (Algeria), Wael Hannach (Tunisia), na Oussam Benyahia (Algeria).

Upande wa VAR atasimama Lahlou Benbraham (Algeria) na Akhona Makalima (Afrika Kusini).
Your browser is not able to display this video.

Dimba la Benjamin Mkapa tayari kwa mechi ya Ufunguzi wa Kombe la TotalEnergies CAF CHAN


Mwonekano wa nje wa Dimba la Benjamini Mkapa kabla ya ufunguzi rasmi wa Kombe la TotalEnergies CAF CHAN 2024


Muziki wa Singeli watambuliwa kama sehemu ya utamaduni, Ufunguzi wa Kombe la TotalEnergies CAF CHAN


Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Mashabiki wakiingia Lupaso watu wameitika ufunguzi CHAN 2024
​
Mashabiki wakiwa wameanza kuingia katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi wa Mashindano ya TotalEnergies CAF CHAN 2024.

Your browser is not able to display this video.
Safari ya Taifa Stars kuelekea uwanja wa Benjamini Mkapa

Your browser is not able to display this video.


​
WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA UFUNGUZI MICHUANO YA CHAN 2024
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 02, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa michuano ya CHAN 2024, katika Dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa ufunguzi Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inachuana na Burkina Faso.




Kikosi cha Taifa Stars
​

Kikosi cha Burkina Faso dhidi ya Tanzania

1. Ladji Sanou
2. Hadalou Sagne
3. Abbas Guiro
4. Franc Tologo
5. Moumouni Diallo
6. Chitou Adjiibade
7. Tertius Bagre
8. Kalifa Nikiema
9. Eleazar Ouattara
10. Souleymane Sangare
11. Nasser Ouattara


Goli la kwanza la mshindano limetoka kwa Abdul Seleman Sopu

HT: Tanzania 1-0 Burkina Faso 45+3 (P).
​
 
Nimeweka Milion moja Taifa Stars Win/draw ole wao wafungwe watanieleza leo
 
Wakuu!

Mechi ya ufunguzi ya na sherehe za ufunguzi kufanyika leo Agosti 2,2025 katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Mechi kali kati Tanzania dhidi ya Burkina Faso inapigwa Saa 2 Usiku.

Je, Taifa Stars kuibeba mabegani Tanzania?
Mkuu mbona umewahi sana? Hii michuano yenyewe mbona ni kama bonanza tu? Kwani mechi saa ngapi?
 
Tanzania dhidi ya mkwe! Dah tabu kweli. Uzuri mkwe halisi ni profdessional hivyoi hawezi kucheza kwenye CHAN ila wakati wa AFCON tutakutana naye.
 
Wakuu!

Mechi ya ufunguzi ya na sherehe za ufunguzi kufanyika leo Agosti 2,2025 katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Mechi kali kati Tanzania dhidi ya Burkina Faso inapigwa Saa 2 Usiku.

Je, Taifa Stars kuibeba mabegani Tanzania?
chan ndiyo vitu gani?
 
Walioitwa kikosini naomba kuwafahamu tafadhali
 
Timu yenyewe ni tia maji tia maji! Ikipata ushindi ni jambo la kushukuru, hata kama sifa zote atapewa Mama Abdul.
 
Reactions: x x
Dstv wanasemaje!? Watarusha. Maana sioni dalili...
 
Wanafanya siasa kwenye mpira na Team Taifa.....kisa kumfurahisha SSH....acha wapigwe hakuna namna.....kocha mbovuuuu
 
Mechi hii inarushwa chaneli zip wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…