FULL TIME || TotalEnergiesCAFCC || Stellenbosch 0-0 Simba SC || Aggreggate 0-1 || 27.04.2025 || 16:00 EAT || Moses Mabhida Stadium

FULL TIME || TotalEnergiesCAFCC || Stellenbosch 0-0 Simba SC || Aggreggate 0-1 || 27.04.2025 || 16:00 EAT || Moses Mabhida Stadium

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
1745700362531.png


Mechi ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika mkondo wa pili kupigwa leo Jumapili.

Mnyama Simba SC atakuwa dimba la Moses Mabhida akicheza na Stellenbosch.

Mnyama anaingia katika mchezo huu akiwa na mtaji wa goli 1 - 0 alilopata kwenye mchezo wa kwanza pale Zanzibar.

Mechi hii itapigwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Karibu kwa live updates

Kikosi cha Simba SC kinachoanza dakika 45 za kwanza
1745755425468.png


Kikosi cha Stellenbosch kinachoanza dakika 45 za kwanza
snapins-ai_3619981976350798958.jpg


Hili ni vibe la Stellenbosch wakiingia uwanjani


Simba SC wakiingia uwanjani wakiwa watulivu wa akili na mwili bila mbwembwe

snapins-ai_3619974871720117741.jpg
snapins-ai_3619974871837348673.jpg
snapins-ai_3619974871652809387.jpg
snapins-ai_3619974871636186082.jpg


KIPINDI CHA KWANZA
  • Mwamuzi anapuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa Mchezo
  • Mchezo unaanza kwa kasi timu zote zikiwa na hamu ya kupata goli la kuongoza
  • Dakika ya 03 Mousa Camara anapangua mpira moja matata na kulicha lango lake likiwa salama
  • Dakika ya 06 Stellenbosch wanakaba kama nyuki
  • Dakika ya 11 Kibu Denis anachezewa madhambi pale ndani ya Box, Refa anafunika mkwaju wa Penati
VAR CHECK - Refa anenda kujiridhisha kupitia VAR
  • Dakika ya 15 VAR CHECK - Hakuna Penati
  • Dakika ya 20 Mukwala anapoteza mpira Stellenbosch wanapiga counter attack Mwamba Camara anaokoa
  • Dakika ya 22 lango la Simba SC ilnakoswakoswa pale wanapoteza nafasi ya kufunga goli Stellenbosch
  • Dakika 25 Stellenbosch wanapata mpira wa kurusha hapa
  • Mpira Mrefu wa kurusha Simba wanaponea chupuchupu hapa
  • snapins-ai_3620014508731748255.jpg

  • Dakika ya 26 Camara anaudaka mpira uliopigwa na De Jong wa Stellenbosch
  • Dakika 35 zimekatika milango bado ni migumu, Stellenbosch wanapeleka moto mwingi lango la Simba
  • 1745761508957.png

  • Lelokoloane anapiga mpira unaokamatwa maridadi na Camara
  • Dakika ya 36 Stellenbosch wanapata Free-kick
  • Dakika ya 37 mpira wa foul unababatiza ukuta sasa ni kona
  • Dakika ya 38 Stellenbosch wanaanza kona fupi hatimaye shout off target
  • Dakika ya 39 Stellenbosch wanapata kona nyingine, lakini inaishia kuwa off targen mpira wa De Jong
  • Dakika ya 41 Baraka Mpenja anasema hii ni mechi ya kucheza kwa akili kwelikweli
Dakika 05 za nyongeza kipindi cha kwanza
  • Dakika ya 45 Simba SC wanapata Free-kick, Ahoua anapigaaaa Simba wanakosa goli hatimaye sasa ni kona
  • snapins-ai_3620035834074868533.jpg

  • +02 Stellenbosch wanaokoa mpira wa kona
  • +03 Stellenbosch wanapata kona Mwamba Camara anatulia na kuunyaka mpira ule
  • +05 Stellenbosch wanapata kona pale yule yule Mwamba Camara analikamata Gozi mikononi mwake
  • Kipindi cha kwanza kimekwisha bado milango ni migumu
TAKWIMU ZA KIPINDI CHA KWANZA. JE, SIMBA WANAPASWA KUFANYA NINI KIPINDI CHA PILI? ENDELEA KUTIRIRIKA KUPITIA COMMENTS
1745762141898.png


KIPINDI CHA PILI

  • Kipindi cha pili kimeanza
  • Dakika ya 50 mechi ni ya moto lakini milango bado ni migumu
  • Dakika ya 51 Stellenbosch wanapata kona lakini hakuna cha maana walichofanya
  • Dakika ya 54 Mohamed Hussein Anashika mpira ndani ya Box Refa anasema ni Penati
VAR CHECK - Refa anaenda kujiridhisha
  • VAR CHECK - Refa anasema hakuna Penati
  • Dakika ya 57 ndugu msomaji mechi ni ya moto kwelikweli
  • Dakika ya 58 Stellenbosch wanakaba kwa nguvu sana katikati ya uwanja
  • Dakika ya 60 Stellenbosch wanapata Free-kick lakini Simba wanaondosha mpira eneo la hatari
  • Dakika ya 61 Stellenbosch wanapata Free-kick tena Simba SC wanaondosha
  • Dakika ya 61 Umiliki wa mpira Stellenbosch ni 53% dhidi ya 47% kwa Simba
MABADILIKO Stellenbosch Daakika ya 64
  • 1745764234614.png
    Screenshot 2025-04-27 172957.png
MABADILIKO Simba SC Daakika ya 65
  • 1745764473969.png

MABADILIKO Stellenbosch Daakika ya 69
1745764527110.png


  • Dakika ya 73 Pressure ipo juu sana milango bado migumuu
  • Mpanzuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu Golikipa anaokoa pale Simba wanakosa goli matata
  • Dakika ya GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Stellenbosch wanapata goli, mechi inaanza upyaaaaaaaaaa...
VAR GOAL CHECK
  • Refa anathibitishahakuna golii Stellenbosch 0 - 0 Simba SC, Ni offside
  • Dakika ya 79 mechi ni ya moto kwelikweli, sijui unaelewaa?????
Dakika 10 zimebaki kutamatisha mchezo

MABADILIKO Stellenbosch Daakika ya 83
Screenshot 2025-04-27 175303.png

  • Dakika ya 86 Moussa Camara anapewa kadi ya njano


MABADILIKO Simba SC Daakika ya 87
  • 1745765481671.png
  • Dakika ya 87 Stellen wanapata kona Camara anaokoa hatari Langoni kwa Simba SC
  • Dakika 90 zimekamilika
DAKIKA ZA NYONGEZA NI +08
  • +02 Camara anapangua shuti moja hatari sana hapa
  • +04 hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake
  • Oya dakika ya +06 Camara anaokoa kwa kudaka maridadi kabisa mpira wa Counter-Attack
WEEEEEEEE REFA MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
SIMBA WANATINGA HATUA YA FAINALIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
FULL TIME
Stellenbosch 0 - 0 Simba SC || Aggreggate ni Stellenbosch 0 - 1 Simba SC
Mshabiki wa Simba SC waliopo hapa Moses Mabhida Stadium wanabubujikwa na machozi ya Furahaaaa hapa, Hatimaye Simba SC sasa atakwenda kukipiga Fainali.
 

Attachments

  • 1745761509526.png
    1745761509526.png
    726.5 KB · Views: 42
  • 1745761738182.png
    1745761738182.png
    726.5 KB · Views: 36
  • 1745764330361.png
    1745764330361.png
    26.6 KB · Views: 40
  • Screenshot 2025-04-27 173152.png
    Screenshot 2025-04-27 173152.png
    26.6 KB · Views: 33
Wale waliokuwa wanajificha kwenye kichaka cha kubeba kombe la medali la mshindi wa pili wanakwenda kuumbuka sasa. Wapo huko Pemba wanashindana kwenye levo zao.
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom