Full Time: UEFA Champions League Final: PSG 5-0 Inter Milan | Mei 31, 2025 - Allianz Arena Stadium

Full Time: UEFA Champions League Final: PSG 5-0 Inter Milan | Mei 31, 2025 - Allianz Arena Stadium

Ozone_

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
505
Reaction score
669
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, zilikuwa ni wiki zikawa siku hatimae ule muda wa kusubiri umeisha na leo ndio ile siku ya kuhitimisha michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu wa 2024/25.

Mtanange wa leo utakuwa baina ya mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG): na washindi wa nafasi ya pili kutoka ligi kuu soka nchini Itali Inter Milan, mtanange ambao utaanza mishale ya saa 4 kamili kwa saa za Afrika ya mashatiki katika dimba la Allianz arena mjini Munich nchini Ujerumani.

Ikumbukwe ya kuwa hii itakuwa fainali ya pili kwa timu ya PSG ikiwa mara ya kwanza ilivheza fainali mwaka 2020 dhidi ya Bayern Munich na kupoteza kwa goli moja bila. PSG wamefika hayua hii baada ya kuwaondosha vigogo wa soka nchini uingereza Arsenal kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.

Kwa upande mwingine timu ya Inter milan itashika dimbani usiku wa leo kutafta taji lake la nne la ligi ya mabingwa barani ulaya huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa fainali dhidi ya wababe toka Uingereza timu ya Manchester city kwa bao moja bila majibu.

Wao wametinga fainali baada ya kuwaondoa watemi kutoka nchini hispania Barcelona kwa jumla ya magoli saba kwa sita.

Je ni Osmane Dembele au ni Lautaro Maryinez kuibuka kidedea usiku wa leo?.
Mimi na wewe hatuna manibu, majibu yatapatikana kuanzia mishale ya saa nne za usiku pale Allianz stadium.

FB_IMG_1748682460849.jpg

06f4896a-db0e-4d52-a437-56ee2153644c.jpeg

1748724354139.png
 
Yani hii fainali ingekuwa Barcelona na Arsenal ndio ingenoga zaidi, anyway may the best team win today japo PSG wajitahidi wachukue tu maana wakishindwa leo, basi kucheza tena fainali sijui hadi mwaka gani bora wenzao Inter tayari hilo kombe wanalo zaidi ya moja
 
Hapa hakuna timu mwenyeji.
Ingekuwa huku kwetu ungesikoa kelele za kina cresentus magori.
Acha Waitwe wazungu
Sometimes huwa inatokea, kumbuka ile fainali ya Bayern dhidi ya Chelsea ilipigwa katika uwanjua huu ambao hutumiwa na Bayern kama uwanja wa nyumbani na bado haikusaidia yeye kubeba kombe.
 
Mziki waliokutana nao liverpool ndio huu anao enda kukutana nao inter. Binafsi ningependa inter abebe ila PSG Nona kama amedhamiria
Hawa jamaa walianza kwa kusuasua sana ila turning point ilitokea baada ya game dhidi ya Manchester city.
Tangia hapo aliekatiza mbele yao alipelekewa pumzi ya moto.
 
Sometimes huwa inatokea, kumbuka ile fainali ya Bayern dhidi ya Chelsea ilipigwa katika uwanjua huu ambao hutumiwa na Bayern kama uwanja wa nyumbani na bado haikusaidia yeye kubeba kombe.
Nakubalana na wewe mkuu.
Kwakuwa hupangwa kabla ya michuano. Inakuaje timu inatangaza viwanja viwili vya mashindano halafu ikiambiwa itumie kiwanja mbadala watu mapovu yanawatoka?
 
Wanadaia Lukaku kawazuia Sana Mambo Yao.
Alizuia Goli dhidi ya City akazingua Fainali za Ndani.
Na juzi kawazuia akiwa na Napoli.
Haya Sasa Timu yenye wa Argentina imepiga timu zenye wa Brazil...and na Chelsea then Spurs Leo tuna Inter na Psg kunabrazil tegemezi.pia ukiangalia

Nakubalana na wewe mkuu.
Kwakuwa hupangwa kabla ya michuano. Inakuaje timu inatangaza viwanja viwili vya mashindano halafu ikiambiwa itumie kiwanja mbadala watu mapovu yanawatoka?
Huu mfumo sio kwetu Afrika tu hata Amerika ya kusini kama sikosei wantumia mfumo wa home and awy hadi fainali.
Ila ukienda Asia wenyewe kuanzia nusu fainali ni game moja tu.
 
Back
Top Bottom