We unajuwa mpira , PSG ni bora kuliko Inter ila Inter wana kitu cha tofauti ambacho kinakunyima uhakika wa kuifunga InterNaiona kama Fainali Bora sana, Kila timu Iko na falsafa tofauti na hii ndio inazidisha utamu wa hii gemu.
Nategemea battle Kali katikati na pembeni mwa uwanja. Nategemea Hakan Calhanoglu, Mkhitaryan na Nicolo Barella watakimbizana sana na kupigana buti na kina Fabian Ruiz, Joao Neves na Vitinha, Leo Nicolo au Hakan au Joao Neves mmoja anaweza kupata kadi hasa njano.
Mendes na Hakimi Leo wana kazi ya ziada hasa defensive, Leo Di Marco na Dumfries watukaja na kuteleza sana kwenye Flanks, ubora mkubwa wa Hakimi na Mendes ni kwenye offensive. Nadhani na naona kabisa kuwa Kvaratshkelia Leo atakuwa ndiye mtu pekee ambaye atawatisha Inter Milan kwenye winga na hii itampa tabu Di Marco, Kvara ni mchezaji mmoja mbaya sana tena sana hasa akivuka nusu uwanja na kuingia ndani.
Lautaro au Thuram watapishana sana kwenye kukaba kama ilivyo kawaida. Nategemea Sub za aina ya kina Fratessi kudectate mchezo. PSG wafanye lolote Leo Fabian Ruiz, Kvichi Kvara wacheze mpira bila hivyo Kwa usongo ninao uona Kwa Inter Milan wanaweza kubeba.
Hapa naona hii game nusu itauliwa Kwa njia mbili ni aidha Quick Transition au Dead ball.
It's tough game. Nusu nyingine ya hii game itaamuliwa na Personality za wachezaji binafsi. Inter wana usongo na ugwadu na hili kombe huku PSG wana hamu.
Team Paris tujuaneHayawi hayawi sasa yamekuwa, zilikuwa ni wiki zikawa siku hatimae ule muda wa kusubiri umeisha na leo ndio ile siku ya kuhitimisha michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu wa 2024/25.
Mtanange wa leo utakuwa baina ya mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG): na washindi wa nafasi ya pili kutoka ligi kuu soka nchini Itali Inter Milan, mtanange ambao utaanza mishale ya saa 4 kamili kwa saa za Afrika ya mashatiki katika dimba la Allianz arena mjini Munich nchini Ujerumani.
Ikumbukwe ya kuwa hii itakuwa fainali ya pili kwa timu ya PSG ikiwa mara ya kwanza ilivheza fainali mwaka 2020 dhidi ya Bayern Munich na kupoteza kwa goli moja bila. PSG wamefika hayua hii baada ya kuwaondosha vigogo wa soka nchini uingereza Arsenal kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.
Kwa upande mwingine timu ya Inter milan itashika dimbani usiku wa leo kutafta taji lake la nne la ligi ya mabingwa barani ulaya huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa fainali dhidi ya wababe toka Uingereza timu ya Manchester city kwa bao moja bila majibu. Wao wametinga fainali baada ya kuwaondoa watemi kutoka nchini hispania Barcelona kwa jumla ya magoli saba kwa sita.
Je ni Osmane Dembele au ni Lautaro Maryinez kuibuka kidedea usiku wa leo?.
Mimi na wewe hatuna manibu, majibu yatapatikana kuanzia mishale ya saa nne za usiku pale Allianz stadium.View attachment 3351936
Nimegundua kuwa dembele nii jamaayangu kabisa.Team Paris tujuane
Watu wanaogopa kupigwa Nondo za Kichwa😂Wakuu nasubiri game hapa gateway annex pub kijichi, ambae yupo around tunaweza kuonana kwa ajiri ya kusalimiana
😀😀😀😀 unamaanisha nini mkuu?Watu wanaogopa kupigwa Nondo za Kichwa😂
ShukraniWale mliopo lindo kama mimi, link hii hapa www.fawanews.com
Hebu nyoosha mkono juu nikuone mkuuWakuu nasubiri game hapa gateway annex pub kijichi, ambae yupo around tunaweza kuonana kwa ajiri ya kusalimiana
Kumbe.Hayawi hayawi sasa yamekuwa, zilikuwa ni wiki zikawa siku hatimae ule muda wa kusubiri umeisha na leo ndio ile siku ya kuhitimisha michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu wa 2024/25.
Mtanange wa leo utakuwa baina ya mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG): na washindi wa nafasi ya pili kutoka ligi kuu soka nchini Itali Inter Milan, mtanange ambao utaanza mishale ya saa 4 kamili kwa saa za Afrika ya mashatiki katika dimba la Allianz arena mjini Munich nchini Ujerumani.
Ikumbukwe ya kuwa hii itakuwa fainali ya pili kwa timu ya PSG ikiwa mara ya kwanza ilivheza fainali mwaka 2020 dhidi ya Bayern Munich na kupoteza kwa goli moja bila. PSG wamefika hayua hii baada ya kuwaondosha vigogo wa soka nchini uingereza Arsenal kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.
Kwa upande mwingine timu ya Inter milan itashika dimbani usiku wa leo kutafta taji lake la nne la ligi ya mabingwa barani ulaya huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa fainali dhidi ya wababe toka Uingereza timu ya Manchester city kwa bao moja bila majibu. Wao wametinga fainali baada ya kuwaondoa watemi kutoka nchini hispania Barcelona kwa jumla ya magoli saba kwa sita.
Je ni Osmane Dembele au ni Lautaro Maryinez kuibuka kidedea usiku wa leo?.
Mimi na wewe hatuna manibu, majibu yatapatikana kuanzia mishale ya saa nne za usiku pale Allianz stadium.View attachment 3351936
Cheki post no 50.Nipen app ya kuchek game