Full Time: Yanga SC 1 - 3 Tabora United | NBC Premier League | Azam Complex | November 7,024

Full Time: Yanga SC 1 - 3 Tabora United | NBC Premier League | Azam Complex | November 7,024

Mechi: Yanga SC VS Tabora United
Ligi: NBC Premier League
Uwanja: Azam Complex
Tarehe: November 7,024
Muda: 🕖 6:00PM
View attachment 3145701


Dakika, 11 Si Yanga wala Tabora hakuna timu iliyopata goli hadi sasa.

Dakika, 15 Mchezo umendelea kuwa mzuri timu zote zinacheza kwa utulivu sana.

Dakika, 19 Tabora wanapata goli kupitia Chikola.

Dakika, 30 Yanga wanaendelea kufanya mashambulizi hadi sasa bado awajapata kusawazisha goli.

Dakika, 34 Mlinda mlango wa Tabora amekuwa bora kudaka mipira hatari kutoka kwa Yanga.

Dakika, 44 Bado ngoma ngumu kwa Yanga hadi sasa. Tabora wakiwa bado wapo mbele.

Dakika 4 zimeongezwa kutamatika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Dakika, 47 Yanga wanapata penati.

Dakika, 48 Tabora wanapata goli la pili kutoka kwa Chikola.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika.

Dakika 45 za kipindi cha pili kimeanza Je Yanga atafanya maajabu ya soka kusawazisha magoli mawili.
Vipi hii page mbona imeganda hivyo hivyo muda sasa?
 
Si mna kikosi kipana au imekuwaje tena, yani kama mpaka timu ndogo kama tabora nayo ni ya kuiwekea first eleven mtatoboa kweli, yani first eleven hiyo hiyo itumike cafcl na nbcpl si watamaliza msimu wakiwa wamechoka sana na kujikuta hawajaambulia kombe hata moja
mkuu umeanza fatilia mpira jana tabora timu ndogo

umecheza nayo haina wachezaji 8 wa kikosi cha kwanza
 
Mleta mada Mkalukungone mwamba

Mbona hauupgate post #1?

Au unaugulia machungu kwanza?
Andika vizuri Faiza,hauupgate ndiyo nini?

Au wewe uto nini umepagawa na kipigo cha ugoko wanachotoa wanangu wa tabora?

Tabora hamieni sasa kupiga hizi spoku maana hazina nyama wameshazeeka Hawa.
20240803_152116.jpg
 
Ndiyo naingia wakuu nini kimetokea!!?
Ni huzuni kuu. Vyura wa pale Jangwani mpaka sasa weshazamishwa kwenye tope umbali wa futi mbili ndani ya tope. Tunasubiri tuone kama wataweza kujitutumua kutoka chini ya hilo tope. Muda waliopewa ni dk. 45 tu, zikiisha hizo wakiwa bado hawajatoka, itakuwa ndiyo kwisha habari yao kwa siku ya leo.
 
Back
Top Bottom