Fumbo la kuku

Fumbo la kuku

0787510341

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
4
Reaction score
0
Pamoja na udhalimu wote ambao kuku anafanyiwa na bidamau bado kuku hajawahi kuuwaza Uhuru wake..!!

Sio kuku tu hata binadamu hajawahi kufikiria kumpatia kuku Uhuru wake ili akaishi mbali kwa amani pasi na hofu ya kisu chake..!

Kwa hifadhi ya mabanda machakavu pamoja na shibe ya masalia ya mwanadamu, inamfanya kuku kujisahau kujenga kiota chake na kufurahia maisha yake kwa aman na Uhuru kama ilivyo kwa ndege wengine huko mwituni...!!

Binadamu hauwazii Uhuru wa kuku kutokana na utamu wa mchuzi wake, nyama pamoja na mayai take. Kwahiyo ni furaha yake kumuona kuku akiendelea kua mdumavu wa fikra na akili yake ili aendelee kumfaidi siku zote za maisha yake..!!

Urithi wa vifaranga wa kuku unabaki kua ni unyonge na utii kwa binadamu huku urithi wa watoto wa binadamu unaendelea kua ubabe mbele ya kuku...!!

Je kuku ni nani katika maadishi haya, na he unadhani ni nani anapaswa kua mkombozi wa kuku ..!!??

naitwa Ditram mwanaharakati..
 
Back
Top Bottom