Fumbo linaloumiza walimwengu ni maisha baada ya kifo

Fumbo linaloumiza walimwengu ni maisha baada ya kifo

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Binadamu huzaliwa, kukua , kuzeeka na baadae kufa kama viumbe wengine...lakini binadamu ndo kiumbe mwenye akili nyingi kuliko viumbe wote duniani, na ndiyo maana Mwenyezi MUNGU alimpa uwezo wa kuitawala dunia na vilivyomo.

Wanasayansi, wataalamu, wavumbuzi, watafiti mahiri na mashuhuri kutoka mataifa yote duniani wameshindwa kuja na jibu linaloeleweka la nini kinafuata baada ya binadamu kufariki dunia.

Hata viongozi wa dini wameshindwa kuthibitisha fumbo hilo gumu duniani.

Wataalamu , Wanasayansi na viongozi wengi wa dini wamekuwa wakitoa majibu yao kwa hisia au ndoto zao...

Sote tunajua, wenzetu hufa kila siku majumbani, mahospitali, ajalini , usingizini, n.k n.k...

Mimi na wewe pia tutakufa kwa namna ambayo hatuijui.

Baada ya binadamu kufa, je

1. Huzaliwa upya ?

2. Huenda kuishi mbingu nyingine kama kiumbe kingine ?

3. Akifa basi amekufa kama ilivyo kwa viumbe wengine, kwamba hakuna kinachoendelea?
 
1 Wathesalonike 4:13-18

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
 
Binadamu huzaliwa, kukua , kuzeeka na baadae kufa kama viumbe wengine...lakini binadamu ndo kiumbe mwenye akili nyingi kuliko viumbe wote duniani, na ndiyo maana Mwenyezi MUNGU alimpa uwezo wa kuitawala dunia na vilivyomo.

Wanasayansi, wataalamu, wavumbuzi, watafiti mahiri na mashuhuri kutoka mataifa yote duniani wameshindwa kuja na jibu linaloeleweka la nini kinafuata baada ya binadamu kufariki dunia.

Hata viongozi wa dini wameshindwa kuthibitisha fumbo hilo gumu duniani.

Wataalamu , Wanasayansi na viongozi wengi wa dini wamekuwa wakitoa majibu yao kwa hisia au ndoto zao...

Sote tunajua, wenzetu hufa kila siku majumbani, mahospitali, ajalini , usingizini, n.k n.k...

Mimi na wewe pia tutakufa kwa namna ambayo hatuijui.

Baada ya binadamu kufa, je

1. Huzaliwa upya ?

2. Huenda kuishi mbingu nyingine kama kiumbe kingine ?

3. Akifa basi amekufa kama ilivyo kwa viumbe wengine, kwamba hakuna kinachoendelea?
Mimi ni Muislamu imani yangu inanieleza kua baada ya kifo kuna maisha ya kaburini kisha tutafufuliwa ili kwenda kuhesabiwa kwa yale matendo tuloyafanya duniani kisha tutalipwa kwa matendo hayo sasa apo ima utaingia peponi au motoni kulingana na Amali zako ulotenda hapa duniani
 
Kula bata mkuu.
Ukifikiria sana mwishowe ujaribu kujinyonha ukizali utazaliwa upya .
La hasha ! jua ndo maxima hivyo
 
Wewe unahofia maisha baada ya kufa? Kuna wengine wanajiuliza, day and night, hivi before walizaliwa, walikuwa wapi KWELI?

Mathematicians wanatuambia kwamba ukipata jibu la ^x,^ otomatikali ^y^ inakuja yenyewe.
 
Sababu ya kifo ndo maana binadamu wanafanya matendo ya ajabu sana mpaka unashangaa
 
Nafikiria kuoza tu daah pozi linaisha
 
maisha ya mwanadamu yameelezwa vyema kabisa kabla hajaja ulimwenguni baada ya kuja , kifo na baada ya kifo mambo yote yameelezwa kwa ufasaha na uwazi kabisa..

(۞ قُلۡ یَتَوَفَّىٰكُم مَّلَكُ ٱلۡمَوۡتِ ٱلَّذِی وُكِّلَ بِكُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمۡ تُرۡجَعُونَ)
Surah As-Sajdah 11

waambie: atakufisheni malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa mola wenu..
 
Back
Top Bottom