Fundi kaniambia gharama zake za kujenga msingi 750,000 ni fair au ananipiga?

Fundi kaniambia gharama zake za kujenga msingi 750,000 ni fair au ananipiga?

Yeye anasema yupo na timu yake ya mafundi wapo kampani... kesho ndo nawaona.. kitajulikana tu
Kwa ujenzi wa kibongo bongo,vijana watakula laki 3 au 2 nyingine aweke mfukoni. Hao hao ndo wataamuwa kuimalisha au kukupiga chenga la macho. Huwezi kujenga bila taarifa. Huko mtaani wanakojenga ukiwapata vijana, wapatane wao,mbona utafurahia kazi na utabaki na karibia nusu!? Usiwabanie tu.

Hata msosi ukipenda wachukulie. Mafundi wanaoeleweka,utawakuta maofisini kwao,na kama nyumba atapatana yote. Msingi, mara lenta, mara nini, hao njaa tu. Kwani wewe ukiamua si unasimamia tu?
 
Kwa ujenzi wa kibongo bongo,vijana watakula laki 3 au 2 nyingine aweke mfukoni. Hao hao ndo wataamuwa kuimalisha au kukupiga chenga la macho. Huwezi kujenga bila taarifa. Huko mtaani wanakojenga ukiwapata vijana, wapatane wao,mbona utafurahia kazi na utabaki na karibia nusu!? Usiwabanie tu. Hata msosi ukipenda wachukulie. Mafundi wanaoeleweka,utawakuta maofisini kwao,na kama nyumba atapatana yote. Msingi, mara lenta, mara nini, hao njaa tu. Kwani wewe ukiamua si unasimamia tu?
Hapo sasa nimekuelewa mkuu, maana yake huyo nayemwita fundi usikute ni mtu wa kati anakubaliana na mimi 750 anaenda tafuta mafundi wa 400 nimekuelewaa hapo lazima walipue kazi
 
Hapo sasa nimekuelewa mkuu, maana yake huyo nayemwita fundi usikute ni mtu wa kati anakubaliana na mimi 750 anaenda tafuta mafundi wa 400 nimekuelewaa hapo lazima walipue kazi
Chukua tu mfano wa rangi na lipu. Mtu atakwambia nakupakia rangi safiiii. Muite tu dalali. Alete vijana anaowajua wazuriiii. Wafanye kazi,asifiwe yeye. Wewe ukizama mtaani,ukaacha uvivu,kule wanakouza rangi kama madukani au zile za mtaani, utawapata wa chap na kazi zao nzuri.

Sawa na ujenzi. Mtu hashiki mwiko,hayupo site,hachanganyi udongo,habebi tofari,eti yeye ni injinia. Dadeki. Kama nyuma ya kawaida ya kuishi,mafundi utapata tu wa bei ndogo ya kibongo. Kama jengo la biashara lina complications,tafuta mtu kwenye ofisi.

Ukiona anakwambia najenga tu msingi,stuka. Engeneer wa kweli kama uko tayari unampa hela anakukabidhi nyumba. Biashara hizo hawawezi.
 
Aisee
Hebu weka ramani, yaani 750,000 mbona ni ndogo sana kwa hii ramani...
1700693321665.png
 
Ni kwa ramani ya vyumba viwili sebule jiko na wash room.

Upana na urefu wa nyumba ni kama mita nane kwa saba na nusu.

Ila pesa ya fundi kaniambia ni 750,000. Sasa kabla sijazama, embu naombeni ushauri maa a mimi ndo mara yangu ya kwanza kujenga.

Hii ni fair ama napigwa? Msingi wenyewe unaweza kula tofali 700 hivi.

Halafu hivi wakiwa site chakula si huwa wanajitegemea wenyewe kutokana na hela yao ama vip?
Kujenga tofali moja ni tsh 300/=, kuchimba msingi wa hicho kibanda tsh 50-80,000. Chakula ni juu yao.
 
Okay mkuu basi nitaangalia... sina uhakika kama ni fundi mzuri ila ameniambia yupo na timu yake...
Kakikisha msingi unainuliwa vizuri, angalau line za tofali juu ya usawa wa ardhi..
Epuka msingi mfupi ambao mtu anaweza kuingia ndani ya nyumba akiendesha BAISKELI🤣🤣🤣

Nyumba yenye msingi mfupi ni nyumba ya kienyeji.

Kitaalam msingi haupaswi kuwa chini ya 45cm yaani ngazi tatu hadi uingie ndani.

So msingi ukiwa ni 60cm nyumba yako itavutia zaidi.
 
Mmmh vyumba viwili, sebule na washroom shilingi 750,000/ kujenga msingi tu?
Unaibiwa kimbia, labda ingekuwa na kuinua boma.
Nimeshuhudia mafundi wanaojenga majengo ya serikali bei za ufundi wanazopewa ni kiduchu sana.
Ingekuwa hivyo serikali isingeweza kupata mafundi wangekuwa wanakimbilia kwa watu binafsi kuwajengea
 
Mbona bei kubwa zana hyo. Hyo ni kazi ya siku mbili tu anaimaliza. Hapo umepigwa kaka shida ya mafundi wana tamaa sana. Mimi huwa ukiniambia bei kubwa kupitiliza hata sitii neno nakwambia nenda nitakuita. Alaf nafunga vioo mazima.. yani watu kibao wako mtaani wanatafuta kazi alaf unapata kazi unampiga mtu bei kubwa hvi
 
Ni kwa ramani ya vyumba viwili sebule jiko na wash room.

Upana na urefu wa nyumba ni kama mita nane kwa saba na nusu.

Ila pesa ya fundi kaniambia ni 750,000. Sasa kabla sijazama, embu naombeni ushauri maa a mimi ndo mara yangu ya kwanza kujenga.

Hii ni fair ama napigwa? Msingi wenyewe unaweza kula tofali 700 hivi.

Halafu hivi wakiwa site chakula si huwa wanajitegemea wenyewe kutokana na hela yao ama vip?
Kiaina imechangamka kutegemea na eneo maana kwa Dar sawa lakini mkoani inaweza kuwa chini tu zaidi ya hapo

Cha msingi relate na bei za fundi mwingine, halafu zingatia ubora
Maana quality ni muhimu kuliko bei kama ni fundi mzuri hata kama anazidi kiwango cha wenzake mchukue huyo huyo
 
Kama boma la bedrooms tatu na vikorokoro vingine linaweza kusimama kwa Milioni 1 mpaka 1.5 basi unaweza kupata majibu kuwa hao mafundi wako bei zao zipo juu unless huo ujenzi una changamoto ambayo siyo ya kawaida ambayo hujaiweka wazi
 
Ni kwa ramani ya vyumba viwili sebule jiko na wash room.

Upana na urefu wa nyumba ni kama mita nane kwa saba na nusu.

Ila pesa ya fundi kaniambia ni 750,000. Sasa kabla sijazama, embu naombeni ushauri maa a mimi ndo mara yangu ya kwanza kujenga.

Hii ni fair ama napigwa? Msingi wenyewe unaweza kula tofali 700 hivi.

Halafu hivi wakiwa site chakula si huwa wanajitegemea wenyewe kutokana na hela yao ama vip?
Naweza kukujibu kua UNAPIGWA na naweza kukujibu kua HUPIGWI.

Iko hivi, kuna gharama za "ufundi" na kuna gharama za "fundi". Kujenga tu msingi wa vyumba vya kulala viwili na labda kuweka mkanda ki kawaida hiyo 750,000/- yaweza kua ni kubwa.

Nimejenga nyumba ya vyumba vinne vya kulala + store, jiko, dining, vyoo kwa msingi wa 600,000/- na ni hapa hapa Dar. Wewe ingefaa hata hamna hamna basi hata 450,000/- umepigwa sana. Hapa nimezungumzia gharama za "ufundi".

Ila pia tusisahau kua kwenye kila sekta kuna "manguli" wake. Hawa bei zao hazishikiki sababu ya majina waliokwishajijengea kwenye sekta zao. Ukiwafuata hawa ukatajiwa bei kubwa huwezi kusema "umepigwa".

Sasa wewe sijui ulimfuata fundi yupi, ndio maana siwezi kusema umepigwa au hujapigwa. Ila unaweza kupata wa bei nafuu ya hapo na akakujengea vizuri tu. Pia kua makini kuna "Saidia fundi/Kondakta" wanaotaka kuhamia kwenye "Ufundi/Dereva", asije kuifanyia nyumba yako majaribio.
 
Ni kwa ramani ya vyumba viwili sebule jiko na wash room.

Upana na urefu wa nyumba ni kama mita nane kwa saba na nusu.

Ila pesa ya fundi kaniambia ni 750,000. Sasa kabla sijazama, embu naombeni ushauri maa a mimi ndo mara yangu ya kwanza kujenga.

Hii ni fair ama napigwa? Msingi wenyewe unaweza kula tofali 700 hivi.

Halafu hivi wakiwa site chakula si huwa wanajitegemea wenyewe kutokana na hela yao ama vip?
Hiyo nyumba ya kuishi miaka 50 mbeleni unaionea ubahiri wa kumlipa fundi 750000.
Lkn uko tayari kubadili kioo cha simu kwa tshs 800000.
Ifikie mahala tujitambue
 
Back
Top Bottom