Fundi kaniambia gharama zake za kujenga msingi 750,000 ni fair au ananipiga?

Fundi kaniambia gharama zake za kujenga msingi 750,000 ni fair au ananipiga?

Ni kwa ramani ya vyumba viwili sebule jiko na wash room.

Upana na urefu wa nyumba ni kama mita nane kwa saba na nusu.

Ila pesa ya fundi kaniambia ni 750,000. Sasa kabla sijazama, embu naombeni ushauri maa a mimi ndo mara yangu ya kwanza kujenga.

Hii ni fair ama napigwa? Msingi wenyewe unaweza kula tofali 700 hivi.

Halafu hivi wakiwa site chakula si huwa wanajitegemea wenyewe kutokana na hela yao ama vip?
*Tofari 700× 300= Tsh 210, 000/=

*Kuchimba msingi= Tsh 60, 000/=

* kumwaga zege(mkanda wa chini)
Tsh 100, 000/=

Jumla tsh 370, 000/=

Wewe ujui kusoma ramani na kuset.kwa iyo hapo kuna ela yake ya kusoma raman na kuset= Tsh 100, 000/=


Kwa iyo ukimpa Tsha 500, 000/= ni sawa
 
Hapo sasa nimekuelewa mkuu, maana yake huyo nayemwita fundi usikute ni mtu wa kati anakubaliana na mimi 750 anaenda tafuta mafundi wa 400 nimekuelewaa hapo lazima walipue kazi
Mkuu mimi ni fundi wacha nikushauri..!!

Kwanza kwa size ya Nyumba yako hiyo pesa sio nyingi kiasi cha kuanza kulalamika...!

Unaweza kuomba Pumbuzo...!

Hayo mambo ya kusema fundi ataleta Vijana waje wafanye kazi then yeye atachukua kingi n.k..... Huo ni Ujinga na kuingilia Majukumu ambayo sio yako, ukimpa mtu kazi, yeye ndo anaamua work plan yake, afanye peke yake na kibarua, ama alete mafundi wengine wamsaidie, hiyo haikuhusu.... Wewe ni kuhakikisha kazi inaenda....!

Kama huna uzoefu na mambo ya ujenzi, usifanye kosa la kukusanya mafundi 5 kila fundi unajua ulipomtoa then waje kufanya kazi pamoja bila msimamizi...!

Mpe fundi kazi, hata kama asipobeba tofari hata moja, ila akaleta mafundi wake na kazi ikawa inaenda hilo ndo Muhimu...!
 
Mmmh vyumba viwili, sebule na washroom shilingi 750,000/ kujenga msingi tu?
Unaibiwa kimbia, labda ingekuwa na kuinua boma.
Nimeshuhudia mafundi wanaojenga majengo ya serikali bei za ufundi wanazopewa ni kiduchu sana.
Ingekuwa hivyo serikali isingeweza kupata mafundi wangekuwa wanakimbilia kwa watu binafsi kuwajengea
Mafundi wa mtàani ni gharama kubwa kuzidi wa miradi ya serikali na mafundi wa makampuni.
Usichokijua ni kwamba mafundi wengi tunajifunzia kazi kwenye hiyo miradi mikubwa. Kule hakuna hasara ya tofali au cement. Ukikosea lawama kwa engineer, foreman, architecturer and so fourth.
Uzuri wa kampuni una uhakika wa kufanya kazi kila siku ijapo malipo ni kiduchu. Huku mtàani malipo ni mazuri lkn hatufanyi kazi kila siku.
Fundi mwenye ufundi wake ataenda kwenye kampuni kujibanza tu japo kwa wiki ili kupoza njaa, lkn sio kuweka kambi.
Yote kwa yote miradi ya serikali na miradi mikubwa inayosimamiwa na contractors malipo hua yanasumbua sana, wew fundi unaweza kupata kidogo tena kwa kuchelewa au usipate had unaondoka!
 
kama upo dar nipe kazi mimi fundi najenga kwa mkono wangu apo kazi za mkoani nilikua naishi tanga 0714442795
IMG_20220129_121122_653.jpg
IMG_20220130_174528_906.jpg
IMG_20220324_181234_501.jpg
 
Swali langu kuu, gharama za ufundi huwa zinapimajwe kwenye ujenzi? Standard zikoje?

Kwa mfano.
-Kuchimba msingi (Urefu, upana, Kimo) mita ni kiasi gani?
-Kufunga mkanda (Urefu, Upana) mita ni kiasi gani?
-Kusuka nguzo na kumimina (Urefu, Upana) kwa mita ni kiasi gani?
-Kusuka nondo za slab, kwa square meter ni kiasi gani?
-Kumimina slab, kwa square meter ni kiasi gani?
-Kumwaga jamzi, kwa square meter ni kiasi gani?
-Kufunga lenta, kwa mita ni kiasi gani?

Note.
Mpaka sasa kupitia JF nimeweza kugundua standard ya gharama hizi za ujenzi.
-Kuweka tiles (wastani wa shilingi 4000 mpaka 5000 kwa square meter moja,)
-Kujenga (Shilingi 300 kwa tofali moja)
 
Anaweza kuwa sahihi kulingana na utendaji wake wa kazi yake maana hatujui huduma zake anatoaje. But nakushauri uingie sokoni kutafuta mafundi stadi maana wapo wengi sana kisha uzungumze nao wakupe bei muafaka. Hiyo ni bei ya juu sana kwa nyumba ya vyumba viwili.
 
Bei ya ujenzi wa nyumba inategemea na location, nature ya ardhi, labour charge , standard ya ujenzi n. K.
 
Back
Top Bottom