Ukisema "mistari hii haina mgongano, kwa sababu hii na hii" kwa kila mistari, nitakuelewa. Nitasoma sababu zako na kuzikataa au kuzikubali kulingana na mantiki yako.
Ukisema "hakuna migongano, migongano unaiona wewe kwa akili yako" bila kutoa uthibitisho kwa nini hakuna migongano, nitakuona mtu anayelazimisha hoja asiyoweza kuitetea.
Mpaka sasa unalazimisha hoja usizoweza kutetea.
Unasema Mungu yupo. Hoja hii hujaweza kuitetea.
Umesema roho ipo, hoja hii hujaweza kuitetea.
Umesema haya maandiko ni matakatifu hayana migongano, hoja hii hujaweza kuitetea.
Kwa sababu.
Mungu hayupo.
Roho hayupo.
Vitabu vina migongano.
Kama unabisha, thibitisha vinginevyo kwa hoja zenye mantiki, si kwa hoja za kulazimisha tu.
Jamani! Si nilikuliza kwa nini unasema mistari hiyo ina migongano? Unaona ugumu gani kuelezea migongano uliyoitaja halafu tukaendelea kujadili?
Ukitoa maelezo ya migongano, itakuwa rahisi kwangu kutoa sababu ya kwa nini nasema sio migongano.
Wewe umeona kuwa ni migongano kwa uelewa wako, mimi sijaona kuwa ni migongano kwa uelewa wangu. Funguka, kwa nini unasema ni migongano.
Hoja zako hazina uzito wa kushindwa kuzitetea. Jitahidi kujibu maswali yanayoendana na hoja zako ili twende sawa. Kuna wakati inabidi nikuulize kwanza kabla ya kutoa jawabu. Sijui kwa nini hupendi kujibu maswali! Katika post # 323 nimekuuliza maswali rafiki sana, lakini hujajibu hata moja.
Sio kweli kwamba nalazimisha hoja nisizoweza kutetea. Ni wewe unayelazimisha hoja ionekane kama ina mantiki. Najibu hoja kutokana na upeo wa akili zangu. Si vinginevyo.
Na vilevile silazimiki kujibu hoja zako kwa kutumia mtazamo wako. Nitajibu kutokana na ufahamu wangu ili upate jibu sahihi kutoka kwangu. Huu ni mjadala, kila mtu na mtazamo wake.
Hoja ya uwepo wa Mungu tumejadili sana lakini hatukumaliza baada ya wewe kung'ang'ania hoja nyingine. Ukakimbilia hoja ya utakatifu wa vitabu badala ya uwepo wa Mungu. Huenda hata hii utaipindua na kuanza hoja nyingine.
Hoja ya uwepo wa Roho, sikumbuki kama tumewahi jadili. Kama unataka, iweke kwenye mjadala.
Kutetea hoja ya migongano ndani ya biblia, sio kazi ngumu kwangu kama utaelezea migongano uliyoiona. Umetaja migongano bila kutoa maelezo ya migongano hiyo. Kutaja na kueleza ni vitu viwili tofauti.