Funzo kwenye mazishi ya Lowassa, andika historia yako mwenyewe usisubiri kuandikiwa, na mwisho wa ubaya ni aibu

Hivi Jk angempambania mwenzake angepungukiwa nini?

Duniani Mambo yote ni ubatili tu, kwenye misiba km hivi ndio unaona Duniani hakuna haja ya kubaniana,yote yanapita tu
Darasani kwangu nilichaguliwa kuwa monitor wa kudumu mpaka tumalize shule. Niliunda mtandao mkubwa wa wapambe/chawa wangu. Niliongoza tani yangu nitakavyo mpaka nikapata changamoto tishio la kuondolewa madarakani. Nikaomba darasa wanikubalie niachie ngazi kwa amani. Mara nikaletewa warithi nisiowaelewa, ikabidi niwapigie kampeni watu wangu mpaka washinde, na walishinda umonita wa kiume na wa kike nikaastaafu kwa raha. Huyu mzee wa msoga asingeshindwa kumpambania mwenzake waliotoka naye mbali kwenye safari ya siasa zao. Alimtosa mwenzake bila aibu, ni dhambi na dhambi humtafuna mtu bila aibu automatically
 
Mkuu, kuna wakati ukipita humu jukwaani unabaki unasikitika tu......walahi imejaa mijinga humuuu, acha kabisa. Tusio na hela ndo tunazidi kuumia mijinga inapoongezeka namna hii maana hatuna sehemu nyingine ya kutoa mawazo zaidi ya jf.....500 tu naperuzi kutwa kucha.

Halafu kuna kitu nakiona, ni kwamba haters wa kikwete kama wanatoka akili kadiri siku zinavyoenda.....we angalia tu mijadala yao humu hususani mada hii; wanakngea hoja nyepesiiiii lakini kwa miguvu mikubwa. Kuna wengine walikuwa wanaheshimika humu lakini taratiibu wanakuwa kama form I (in terms of thinking).

Uzuri kikwete anawajulia sana hawa wapuuzi, hawajibu na wala haangaiki nao...kesho au keshokutwa ( kama uhai upo) utamuona anatabasamu anaendelea na hamsini zake. Hii mihaters ndiyo inayobaki ikichujuka kwa hasiea na wivu.
 
Hebu sikilizeni kituko hiki wadau! Dah, ngoja nijitokee humu nisije nami nikawa tahira bure. Jioni njema!!
 
History ya marehemu anayeianda si familia ya marehemu!

Historia haiandaliwi na familia maani ni uhalisia wa maisha yako, ila wasifu ndio huandaliwa na familia ya marehemu. Humo ndio familia huweka watakacho kwa utashi wao, au kwa shinikizo la nje ya utashi wao.
 
Naunga mkono hoja
 
Kiuhalisia huo ndiyo uhalisia na ukweli ila kibongo ni bifu.

Ukitaka ugomvi na mtanzania mweleze ukweli.
 

Unakuta mtu yupo Kizimkazi huko anakuja kulalama humu kuwa Kikwete alimsaliti Lowassa, ukiuliza alimsaliti kwenye nini, hakuna majibu ya kueleweka.

Kilichotokea Baina ya Kikwete kilipangwa kitokee, na wanaojua hasa ni Kikwete na Lowassa. Hata angesifiwa Kikwete leo, isingebadili ya kile kilichotokea.

Familia inalalamika Lowassa kunyimwa Haki yake ya Matibabu kama kiongozi mstaafu, lakini Bado analaumiwa kikwete badala ya Jiwe.

Lowassa alikuwa msafi kiasi kumzidi Magufuli? Wagombea walikuwa kama 40 hivi, ni wangapi walihama Chama baada ya kukosa nafasi?

Kuna wakati MUNGU anaamua kuonesha Jambo baada ya kujikuta una haki zaidi kwenye Jambo hilo na ndicho kilichotokea kwa Lowassa, kwa kutumia fedha alizoiba kwa watanzania alijikuta ana haki ya kuwa Rais wa Nchi ila MUNGU hakupanga hilo.
 
Lowassa alikuwa na nia njema kwa taifa hili, ila maslahi yake binafsi yalikuwa mbele zaidi ya maslahi ya taifa na hiyo ndiyo iliyokuwa wekaness kubwa sana kwake. Msuguano binafsi dhidi ya Kikwete ni jambo jingine kabisa, ila Lowassa alipokuwa Waziri wa ardhi (Chini ya Ali Hassan Mwinyi) alichukua hatua nyingi sana zilzlizokuwa na sura za Uzalendo wakati mfaidika mkubwa akiwa ni yeye mwenyewe Lowassa. Tabia hiyo ilibaki akilini mwake miaka yote hadi pale ilipofikia kuwa ndoto ya urais haipo tena.
 


Mke wangu ana mtazamo kama wako, ila laiti angelijua, angekufa na presha, Usiseme hayo maneno kuhusu mumeo, unaeza dondoka na usiamke
 
Mungu yupi huyo kwenye taifa lililojaa dhuluma, ufisadi na ukosefu wahaki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…