Hivi kwanini Lowassa asingeanza kwanza yeye kugombea Urais halafu awamu inayofuata ndo iwe ya JK?
Lowasa ndio alikuwa bingwa wa mikakati, unapokuwa king maker hauna pressure ya kutangulia kwenye jahazi, unaingiza kwanza raia Wako.
Lowasa ndiye alisimamia kuhakikisha Samuel Sitta anashinda uspika, mchuwano ulikuwa ni mkali sana Lowasa alisambaza jina la Samuel Dodoma nzima jina likawa kura ni Kwa Six yani Sitta, kila unayekutana naye unaambiwa ni Six, Six, Six.
Ndio maana issue ya Richmond Lowasa ilimuuma sana kwani alianza kusalitiwa na spika Sitta ambaye ni Lowasa ndiye aliongoza kampeni za kumuweka madarakani, lakini za ndani kabisa Sitta alikuwa anautaka Uwaziri mkuu Kabla hawajampooza kumpa uspika.
Ndio maana Lowasa kwenye speech yake alisema anajuwa tatizo ni uwaziri mkuu, let me grant their wish, hili lilikuwa ni dingo direct Kwa Samuel Sitta na ndio maana Lowasa alipojiuzuru bungeni Samuel Sitta akapigwa na butwaa na yeye kama spika akaomba muongozo, hakuna aliyetegemea kama Lowasa anaweza kuachia ngazi.
Samuel Sitta alikuwa na uwezo wa kumlinda mshirika mwenzao Lowasa Kwa kutounda Kamati ya Mwakyembe na hata ilipoundwa alikuwa na uwezo wa kuzuia report isisomwe na Jk alikuwa na uwezo wa kuneutralise mambo, lakini hamna, ni ukweli mtupu Lowasa alisalitiwa na washirika wake na ndio maana baadaye hata Kingmaker himself Rostam Aziz aliamuwa kuachana na Siasa uchwara Kwa kuachia ngazi.
Kama tunaiba tuibe wote usnitch haufai, ndio hawa kina JK wote majizi baadaye yanajichenga yaonekane waadilifu wakati si kweli.