Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

Mkuu, huyu ameshindwa kuandika ukweli, kilichomfurumusha huyo Raisi wa Mali ni kushindwa kudhibiti ufisadi ndani ya nchi yake, Jeshi likaona haina Maana kuwa wajeda waendelee kuona wizi ukitamalaki Wakati raia wengi wa nchi hiyo wanaishi maisha ya mateso na dhiki Ili Hali Utajiri wa nchi Yao ukigawanwa na wachache

Sasa anapokuja kulinganisha na hapa, Kwa kigezo kipi mpaka aseme Eti ni Bora hata hapa kufanyike kama Mali,

Nchi inavyojengwa kiasi hicho, kila mtu anaishi Kwa nguvu zake yeye mwenyewe, na Pesa inayopatikana inaonekana inafanya vitu, mafisadi wamebanwa mbavu hawapumui, Raisi aliyepo Sio pandikizi ni Mtanzania aliyewekwa na Watanzania,

Kwanza hao mapandikizi ndio inabidi wakataliwe kote Africa Ili Africa isonge mbele

Yawezekana umepokea ujumbe tufauti na makusudio yangu. Labda nikuulize, wadhani Rais Magufuli siyo fisadi? Ikiwa ni msafi mbona anazuia Mkuguzi Mkuu kukagua baadhi ya taasisi na mashirika ya umma likiwamo ATCL? Anaficha nini? Kinachomsaidia kwa sasa ni kwamba amefanikiwa kuuaminisha umma kwamba yeye ni msafi na kwamba anapambana na ufisadi. Sasa wewe endelea kuamini hivyo hivyo. Hivi ulifurahishwa na ununuzi wa wabunge wa upinzani? Wadhani halikuwa agizo la Rais Magufuli?

"Sasa anapokuja kulinganisha na hapa, Kwa kigezo kipi mpaka aseme Eti ni Bora hata hapa kufanyike kama Mali" - hii sentesi yako inaukakasi, mimi sijasema ni bora Tanzania ifanyike kama Mali, nilichoandika ni kuwaasa maafisa wandamizi wa serikali kufanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria maana hawaijui kesho yao.

"Nchi inavyojengwa kiasi hicho, kila mtu anaishi Kwa nguvu zake yeye mwenyewe, na Pesa inayopatikana inaonekana inafanya vitu, mafisadi wamebanwa mbavu hawapumui, Raisi aliyepo Sio pandikizi ni Mtanzania aliyewekwa na Watanzania," - ujenzi unaouongelea upe miaka 5 pekee, hakuna ubora wowote.
 
Hivi ulifurahishwa na ununuzi wa wabunge wa upinzani? Wadhani halikuwa agizo la Rais Magufuli?
Nimeishia hapa Kusoma, na nimegundua kuwa Huna hoja Bali unachuki?

Jenga hoja mkuu, usiweke hisia zako tu na jinsi ulivyosikia kutoka Kwa watu, ukiambiwa utoe ushahidi utaweza?
 
Kilichotokea nchini Mali na nchi mbalimbali duniani kuhusu viongozi madikteta kuondolewa madarakani kinatoa somo kwa maafisa waandamizi wa serikali ya Tanzania kwamba kwa kuwa hawaijui kesho yao basi ni vema kutenda haki na usawa kwa watu wote bila kujali vyama vyao vya siasa kwa kufuata katiba na sheria za nchi.

Ni bora kujiuzulu ikiwa agizo la Rais linapingana na katiba na sheria za nchi kuliko kushiriki katika uovu ambao utakuja kuwagharimu siku za usoni siku ambapo mnayemtetea mbele za watu hatokuwa na nguvu ya kuendelea kuwalinda.

Heshimuni vyama vyote vya siasa kwa mujibu wa katiba na sheria kwani leo ni CCM kesho ni CHADEMA. Dunia inakwenda kwa kasi sana na mabadiliko ya upepo wa kisiasa ni suala la siku moja tu.

KWA LEO NI HAYO TU, NAWATAKIA SIKU NJEMA

Mali kuna matatizo makuu matatu, uchumi mbovu, Ufisadi na kukua kwa Ugaidi.

Raisi wa nchi hiyo Ibrahim Baubacar Keita ameshindwa kuiongoza nchi hiyo akiwa amezungukwa na UN, mkoloni wa zamani Ufaransa na makundi ya kigaidi.

Mapinduzi yalotokea wakati huu si ya kwanza kwani kama wafuatilia kulitokea mapinduzi kama haya mwaka 2012, ambapo wanajeshi wakitokea katika kambi hiyohiyo ya Kati, walifanya mapinduzi ambayo yalifanya kuwepo na "power vacuum" na magaidi wakashika sehemu kubwa ya kaskazini.

Nchi hii ina shida kubwa ya ugaidi na sasa hivi kuna tatizo la COVID-19 ndo imekuwa balaa.

UN tangu 2013 ina wanajeshi wapatao 15,600 wa kulinda amani.

Atakuwa ni mtu mjinga pekee atakaelinganisha matatizo ya Mali na nchi ya amani na Utulivu ya Tanzania.
 
Ecowas wapumbavu Sana Ni sawa na umoja wa afrika ndio wanayoyasopoti madikteta ili kuuwa watu wao, Kama wananchi awamtaki kiongozi wao kwann wanawalazimisha
 
Kilichotokea nchini Mali na nchi mbalimbali duniani kuhusu viongozi madikteta kuondolewa madarakani kinatoa somo kwa maafisa waandamizi wa serikali ya Tanzania kwamba kwa kuwa hawaijui kesho yao basi ni vema kutenda haki na usawa kwa watu wote bila kujali vyama vyao vya siasa kwa kufuata katiba na sheria za nchi.

Ni bora kujiuzulu ikiwa agizo la Rais linapingana na katiba na sheria za nchi kuliko kushiriki katika uovu ambao utakuja kuwagharimu siku za usoni siku ambapo mnayemtetea mbele za watu hatokuwa na nguvu ya kuendelea kuwalinda.

Heshimuni vyama vyote vya siasa kwa mujibu wa katiba na sheria kwani leo ni CCM kesho ni CHADEMA. Dunia inakwenda kwa kasi sana na mabadiliko ya upepo wa kisiasa ni suala la siku moja tu.

KWA LEO NI HAYO TU, NAWATAKIA SIKU NJEMA

Serikali ya CCM haiamini kama inaweza kutokea kwa TZ ,Kuanzia DGIS ,IGP,CDF wote wanalamba miguu ya MEKO kwahiyo hawawezi kuasi maana pia wanafaidika sana na MFUMO huu.
 
CreativityCode,
Unapoteza muda tu! Kwa akili yako unaamini Tz iko kundi la nchi kama hiyo Mali? Unaijua Mali au unadandia kila kinachojitokeza? Someni muongeze uelewa badala ya kila siku kuhangaikia whatsapp!
Vizazi ubadilika watz wa Jana sio wa Leo
 
Serikali ya CCM haiamini kama inaweza kutokea kwa TZ ,Kuanzia DGIS ,IGP,CDF wote wanalamba miguu ya MEKO kwahiyo hawawezi kuasi maana pia wanafaidika sana na MFUMO huu.
Ni kwa sababu wamekariri pia ni wanufaika,ongea na wa chini yao usikie mawazo yao wanawalaumu wananchi ndo wajinga wanawachelewa pa kuanzia.
Huwa wananchi ndo uanza wao uja kumaliza mchezo
 
Ecowas wapumbavu Sana Ni sawa na umoja wa afrika ndio wanayoyasopoti madikteta ili kuuwa watu wao, Kama wananchi awamtaki kiongozi wao kwann wanawalazimisha

Kosa na ECOWAS ni lipi?
 
Kupinga maamuzi ya wananchi ya kumktaa Keita,

Wananchi wa Mali wamemchagua Keita mara mbili!!

Na huyu ana support yote ya mabeberu akiwemo mkoloni wa zamani Ufaransa na wengine kama USA.

Sasa unaposema wananchi wamemkataa unatumia vigezo vipi.

Wanajeshi wamemwondoa raisi amechaguliwa kihalali na wananchi wa Mali mara mbili.
 
Wananchi wa Mali wamemchagua Keita mara mbili!!

Na huyu ana support yote ya mabeberu akiwemo mkoloni wa zamani Ufaransa na wengine kama USA.

Sasa unaposema wananchi wamemkataa unatumia vigezo vipi.

Wanajeshi wamemwondoa raisi alichaguliwa kihalali na wananchi wa Mali.
Hayo maandamano ya kumpinga nao 4 months ya nn Sasa Kama wanampenda
 
Hayo maandamano ya kumpinga nao 4 months ya nn Sasa Kama wanampenda

Maandamano ya kutengenezwa ni kiinimacho tu kuonyesha wananchi wanataka masuala fulani lakini kuna hila nyuma yake.

Kwamza uchaguzi wa 2013 alishinda kwa 77% hiyo ni ushahidi tosha kwamba wanachi wa Mali wana imani nae.

Ni maandamano ambayo yanaratibiwa na wanaojiita wapinzani ambao wanataka kuendelea kunufaika na "Chaos" iliyopo ya ugonjwa wa COVID-19, na Ugaidi unaoendelea( kumbuka magadi walivamia hoteli ya kitalii majuzi).

ECOWAS ina wanachama 15 ikiwemo Mali hivyo haiwezi kuvumilia kuona raisi aliechaguliwa kihalali kupitia sanduku la kura anapinduliwa na kikundi cha wanajeshi wachache wenye uchu wa madaraka.

Ndio maana ECOWAS imefunga mipaka na kuzuia mizunguko ya fedha inayoihusisha Mali.
 
Hivi kwa utawala huu wa awamu ya 5 kama utaendelea hivi unafikiri hatutaingia road?
Yaani kuna wajinga wanaamini hizi Sheria kandamizi zinazotungwa kumsifia Rais tutazivumilia tu? Haiwezekani nchi yote itungiwe Sheria za kumuona binadamu mmoja ni bora sana kuliko wengine mtarajie muwe salama milele, kwa taarifa yenu hata huko mnokoona yanatokea kuna watu hawakuwahi kuota hiyo ndoto mpaka waliposhuhudia kwenye runinga malaika wao kala pingu ndio wakaamini.
 
Back
Top Bottom