Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

Kumbuka kuna tofauti kubwa Kati ya wasanii na waigizaji,Wasanii hapa Tanzania wamebaki Prof.J na shugu,na marehemu J.Komba. nyie wote ni waigizaji.
Duh,kwanini mkuu?
 
Wajumbe wamemfanya anko wangu kukosa hamu ya kula.
juzi kavaa shati nje ndani,kasahau hata funguo za gari aliweka wapi.

Halafu hiyo ccm inayogawa rushwa kama njugu, ndio ilikuwa inahadaa wananchi kuwa serikali ya chama chao imetokomeza rushwa ndani ya miaka mitano. Bahati nzuri Mungu hamfichi mnafiki, kumbe walikuwa wampaka rais mafuta kwa mgongo wa chupa. Niliwahi kusema, ukisema kiongozi anajisifu kupambana na rushwa, lakini hataki uhuru wa vyombo vya habari na uwazi jua huyo ni tapeli kama matapeli wengine.

Huyu mgombea anayelialia hapa kuhusu rushwa, ni baadhi ya wananchi walioingia hadaa ya hizi propaganda mfu, kuwa ccm imetokomeza rushwa, akaingia kichwa kichwa akidhani anachohubiriwa ndio chenyewe. Saa hii kagundua kuwa ccm ni ile ile. Paskali Mayalla na yeye ni baadhi ya watu waliokubali Hadaa ya ccm, naye akapata kura moja kisa hana hata 10. Alidhani hizi mada anazoleta hapa jukwaani na kujiita mzalendo ndio zitambeba. Kumbe wajumbe walikuwa wanamchora tu.
 
Kamuulize Mzee wa K-vant kapewa kiasi gani cha fedha na Nyalandu.
alafu pia akwambie na kiasi cha fedha alichopewa na Edlow 2015.

Ndio umemaliza utetezi wa hii rushwa ya aibu mliyokuwa mnahadaa wananchi kuwa Magufuli anapambana nayo?
 
Mkuu njoo huku iboya tufanye biashara ya mbao, tuachane na siasa
 
Binafsi sijapendezwa na huu mstari "Diwani aliyekuwa akitetea kiti hana siasa zenye manufaa hata kidogo,kwa ufupi tu ni mzee,ameishia darasa la 4,si mzawa wa ile kata na mpaka sasa aslimia 80 ya shughuli na makazi yake yapo nje ya kata yetu".
Hiyo ni sawa na unamtongoza binti na kwakua unamfahamu bwana wake, basi unaanza kumpondea kwa binti.
Yaani kwa aina hiyo ya kampeni, hata hiyo kura 0 walikupendelea na ilitakiwa uambiwe kura zako ni zile zilizo haribika.
 
Ndio umemaliza utetezi wa hii rushwa ya aibu mliyokuwa mnahadaa wananchi kuwa Magufuli anapambana nayo?
JPM wala hakubaliani na rushwa. Ndio maana chama kimeweka utaratibu wa kuwachuja upya wagombea ili kuwaondoa watoa rushwa.

na wagombea wengine waliopita wapo mikononi mwa takukuru na kamati kuu itawaengua.
 
JPM wala hakubaliani na rushwa.ndo maana chama kimeweka utaratibu wa kuwachuja upya wagombea ili kuwaondoa watoa rushwa.
na wagombea wengine waliopita wapo mikononi mwa takukuru na kamati kuu itawaengua.

Hakubaliani na rushwa kisha hakuna mtu mahakamani? Takukuru ni magereza mpaka watu wawe mikononi mwao? Huko kwenye kamati kuu wataenguliwa kina team Membe, na wale ambao hawatakuwa sehemu ya ajenda ya kumuongezea rais muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
 
JPM wala hakubaliani na rushwa.ndo maana chama kimeweka utaratibu wa kuwachuja upya wagombea ili kuwaondoa watoa rushwa.
na wagombea wengine waliopita wapo mikononi mwa takukuru na kamati kuu itawaengua.
Katika hili nakuhakikishia mkuu,Kuna zaidi ya asilimia 80 wote,waliopata kura nyingi wamezipata kwa rushwa tupu,wale waliopata sifuri au hata 5 ndo hawakutoa rushwa hata kidogo,Kama chama kinataka kutokomeza rushwa kwenye uchaguzi,basi wanapaswa kufanya maamuzi magumu mno Tena mno ili kupitia sifa za hata wale waliopata 0 maana hao ndio waadilifu lakini pia hawana makundi ili kutoa funzo kwa chaguzi zijazo.

Namuonea Sana huruma mheshimiwa Rais,Ana Nia nzuri kwa Tanzania kwa kutokomeza rushwa,lakini masikini ya Mungu juhudi zake zinahujumiwa mno na wachini wake.

Hakika bado tuna safari ndefu mno.
 
Pole sana mtia nia, ila ulikuwa unakutana na wajumbe ukitokea wapi? Penye udhia penyeza rupia ndg!
Funzo kuu ulitakiwa utambue kuwa CCM ina wenyewe bila kujali ni STD 4 au 7!!
 
Magufuli kaikuta rushwa ishakuwa na mizizi mirefu mno.kuing'oa pia ni mchakato wa mufa mrefu sana.

Kimsingi hapambani na rushwa, ndio maana ni adui wa vyombo vya habari, na demokrasia kwani akiruhusu hayo mambo, taarifa za rushwa zitakuwa hadharani. Hivyo alichofanya ni kuhakikisha habari za rushwa hazitangazwi, ili ahadae watu kuwa anapambana na rushwa kwa ajili ya kusaka sifa za kisiasa. Makada wa chama chake kwa kuwa wanajua hamna hiyo vita bali maigizo, ndio maana wanatoa rushwa bila woga.

Ingekuwa kweli anapambana na rushwa, leo hii kungekuwa na wanaccm sio chini ya 1,000 mahakamani, na kwa uchache kabisa 200 wangefungwa. Kinyume na hapo, anajiandaa kubaka box la kura ili watangazwe wabunge wa ccm, na kuwa na bunge la wala rushwa, ambao atawatumia kupitisha ajenda yake ya kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
 
Ndiyo tabia zenu
Hahaaaaa,haipo hivyo mkuu,majukumu ya ajira yanafanya kwa kiasi Fulani kutoshirikiana kila Jambo na hao wajumbe na hivyo kuonekana Kama tunawadharau kumbe sivyo.Lakini kwakuwa nimejifunza kitu,2025 nitakuwa mtu tofauti na 2020.
tapatalk_1595659759521.jpeg
 
Binafsi sijapendezwa na huu mstari "Diwani aliyekuwa akitetea kiti hana siasa zenye manufaa hata kidogo,kwa ufupi tu ni mzee,ameishia darasa la 4,si mzawa wa ile kata na mpaka sasa aslimia 80 ya shughuli na makazi yake yapo nje ya kata yetu".
Hiyo ni sawa na unamtongoza binti na kwakua unamfahamu bwana wake, basi unaanza kumpondea kwa binti.
Yaani kwa aina hiyo ya kampeni, hata hiyo kura 0 walikupendelea na ilitakiwa uambiwe kura zako ni zile zilizo haribika.
Hayo ni maneno ya wapiga kura mkuu,mpaka Leo wanaendelea kusema hivyohivyo,Wala haikuwa sehemu ya Sera yangu. Nisieleweke vibaya tafadhali kwamba ni siasa za taka maji kihivyo,lengo la kuyaandika maneno hayo hapa ni kuonesha namna wapiga kura walivyokuwa wakitulaghai kwa maneno hayo na ndo maana nimehitimisha kwa kuweka funzo nililolipata katika mchakato huo.
 
Katika hili nakuhakikishia mkuu,Kuna zaidi ya asilimia 80 wote,waliopata kura nyingi wamezipata kwa rushwa tupu,wale waliopata sifuri au hata 5 ndo hawakutoa rushwa hata kidogo,Kama chama kinataka kutokomeza rushwa kwenye uchaguzi,basi wanapaswa kufanya maamuzi magumu mno Tena mno ili kupitia sifa za hata wale waliopata 0 maana hao ndio waadilifu lakini pia hawana makundi ili kutoa funzo kwa chaguzi zijazo.

Namuonea Sana huruma mheshimiwa Rais,Ana Nia nzuri kwa Tanzania kwa kutokomeza rushwa,lakini masikini ya Mungu juhudi zake zinahujumiwa mno na wachini wake.

Hakika bado tuna safari ndefu mno.

Nia nzuri ya kupambana na rushwa haipo kwenye mdomo, bali ipo kwenye vitendo. Zaidi ya asilimia 90 ya waliohama upinzani kwenda kuunga juhudi walipewa rushwa ya fedha, na ahadi ya kurudishiwa vyeo vyao. Na chaguzi zote za marudio ziligubikwa na ushenzi wa kiwango cha juu ili kuwarejesha hao waliohama kuunga mkono juhudi. Na yote hayo yalikuwa ni maagizo yake.

Wenye ccm rushwa hiyo wameijua vizuri, ndio maana na wao wameamua kufanya hivyo hivyo, na yeye hana la kuwafanya maana ukweli uko wazi. Hakuna mtu dunia hii anapambana na rushwa kwa kufanya rushwa, kudhibiti vyombo vya habari na kuua demokrasia. Ukiona mtu wa hivyo halafu aseme anapambana na rushwa, ujue huyo ni tapeli kama tapeli mwingine yoyote. Rushwa, mbeleko ya vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi, ndio sababu kuu tatu za ccm kuendelea kuwa madarakani hadi leo.
 
Mkuu nasikia kuna dogo anafanya kazi Ikulu na ni rafiki yake msigwa msemaji wa Ikulu ndio ameongoza kura za maoni huko kwenye Jimbo lenu la Wangingombe nae katoa rushwa??
 
Katika hili nakuhakikishia mkuu,Kuna zaidi ya asilimia 80 wote,waliopata kura nyingi wamezipata kwa rushwa tupu,wale waliopata sifuri au hata 5 ndo hawakutoa rushwa hata kidogo,Kama chama kinataka kutokomeza rushwa kwenye uchaguzi,basi wanapaswa kufanya maamuzi magumu mno Tena mno ili kupitia sifa za hata wale waliopata 0 maana hao ndio waadilifu lakini pia hawana makundi ili kutoa funzo kwa chaguzi zijazo.

Namuonea Sana huruma mheshimiwa Rais,Ana Nia nzuri kwa Tanzania kwa kutokomeza rushwa,lakini masikini ya Mungu juhudi zake zinahujumiwa mno na wachini wake.

Hakika bado tuna safari ndefu mno.
Safari ni ndefi sana.rushwa imetamalaki waziwazi,tena watoaji na wapokeaji wala hawana hofu kabisa.
 
Back
Top Bottom