Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

Binafsi sijapendezwa na huu mstari "Diwani aliyekuwa akitetea kiti hana siasa zenye manufaa hata kidogo,kwa ufupi tu ni mzee,ameishia darasa la 4,si mzawa wa ile kata na mpaka sasa aslimia 80 ya shughuli na makazi yake yapo nje ya kata yetu".
Hiyo ni sawa na unamtongoza binti na kwakua unamfahamu bwana wake, basi unaanza kumpondea kwa binti.
Yaani kwa aina hiyo ya kampeni, hata hiyo kura 0 walikupendelea na ilitakiwa uambiwe kura zako ni zile zilizo haribika.
Kwamba jamaa alitakiwa kutolewa ukumbini kwa makofi na mieleka kabisa au??[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu nasikia kuna dogo anafanya kazi Ikulu na ni rafiki yake msigwa msemaji wa Ikulu ndio ameongoza kura za maoni huko kwenye Jimbo lenu la Wangingombe nae katoa rushwa??
Aliyeongoza Wanging'ombe ni ENOCK KISWAGA, nimepata fununu hizo kwamba katoa rushwa na eti mbunge aliyekuwa akitetea nafasi bwana Lwenge amemkatia rufaa,ukweli ni kwamba hata yeye Lengwe amemwaga Sana hela lakini kazidiwa kete,lakini ndo hivyo mwizi akiibiwa basi mtaa mzima utajua.
 
Hakubaliani na rushwa kisha hakuna mtu mahakamani? Takukuru ni magereza mpaka watu wawe mikononi mwao? Huko kwenye kamati kuu wataenguliwa kina team Membe, na wale ambao hawatakuwa sehemu ya ajenda ya kumuongezea rais muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
Sundi + Kivuko etc?
 
Sijavunjika Sana moyo na sirudi nyuma,dhamira ya kuwatumikia wananchi bado ipo hata kwa awamu nyingine huku nikisahihisha makosa yaliyonigharimu awamu hii,nitamuunga mkono yeyote atakayeteuliwa na chama,Wala sihami chama.
Hongera sana kwa kujifunza siasa kwa vitendo. Next time wewe panda dau zaidi ya wote. It is not rocket science kwani hii ndio modus operandi ya CCM kuanzia kwenye ngazi ya Ubalozi.

Sasa wewe unaishi town unakula bata na unataka uibukie tu kule kupewa kura na wajumbe dakika za mwisho, tena ukiwa na kichwa chako tu? Pole na hongera. I hope salary yako ya July nayo haijapigwa spanner.
 
Kamuulize Mzee wa K-vant kapewa kiasi gani cha fedha na Nyalandu.
alafu pia akwambie na kiasi cha fedha alichopewa na Edlow 2015.
Nikuulize wewe maana utakua unajua hebu tambie walimpa kiasi gani?
Maana kila mtu anajua jinsi ubunge na udiwani huupati bila kutoa rushwa ndani ya CCM.
 
Hongera sana kwa kujifunza siasa kwa vitendo. Next time wewe panda dau zaidi ya wote. It is not rocket science kwani hii ndio modus operandi ya CCM kuanzia kwenye ngazi ya Ubalozi.

Sasa wewe unaishi town unakula bata na unataka uibukue tu kule kupewa kura na wajumbe dakika za mwisho, tena ukiwa na kichwa chako tu? Pole na hongera. I hope salary yako ya July nayo haijapigwa spanner.
Ahsante mkuu, nimejifunza kwa vitendo,na salary nimepata.
 
Nikuulize wewe maana utakua unajua hebu tambie walimpa kiasi gani?
Maana kila mtu anajua jinsi ubunge na udiwani huupati bila kutoa rushwa ndani ya CCM.
Walimpa kiasi cha kutosha kuondoa makengeza.
 
Hongera mkuu CCM yote inanuka rushwa na hivyo maendeleo ya nchi hii tutasikia Kenya tunasema kila siku angalau tupunguze huu utopolo lazima tuwe na katiba mpya ambayo itaweka misingi ya maendeleo kuanzia kwenye serikali,mahakama,pamoja na bunge ,sasa wewe fikiria wabunge 300 wamehonga wajumbe ili wapate ubunge hivi tunakwenda wapi kama taifa? Hongera kwa kujaribu
Tatizo jingine wanaotoa mapendekezo ya sheria pamoja na kura za kuipitisha hiyo katiba mpya 95% hawajaingia kwa njia halali.. usitegemee kama watajichinja hata siku moja..Kikubwa pambana na maisha yako! Pambana na hali yako!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zifahamu Lugha na kauli za Wajumbe

"tupo pamoja" "tupo nyuma yako" "unakubalika sana" "umeeleweka sana" "sifa zako zilitangulia kabla yako hata huna sababu ya kuongea nasi" "wewe ni jembe", "wapinzani wako wanataka kupima kina cha maji kwa miguu miwili", "Wee mtu wetu sana tena wa nyumbani kabisaa", "mzawa"... "marehemu Babaako tumeishi nae vizuri sana kipindi yupo hai"..."wee ndio chagua letu", "Wewe ni mtu wa watu".. "Huna makuu".. "Usihofu".. "Tunasimama na wewe",.. "wewe ndio mtu wetu hatutaki mwingine.."
 
Zifahamu Lugha na kauli za Wajumbe

"tupo pamoja" "tupo nyuma yako" "unakubalika sana" "umeeleweka sana" "sifa zako zilitangulia kabla yako hata huna sababu ya kuongea nasi" "wewe ni jembe", "wapinzani wako wanataka kupima kina cha maji kwa miguu miwili", "Wee mtu wetu sana tena wa nyumbani kabisaa", "mzawa"... "marehemu Babaako tumeishi nae vizuri sana kipindi yupo hai"..."wee ndio chagua letu", "Wewe ni mtu wa watu".. "Huna makuu".. "Usihofu".. "Tunasimama na wewe",.. "wewe ndo mtu wetu hatutaki mwingine.."
Hahahaaaaaaa, umeua kabisa mkuu.
 
Hahaaaaa,Kama inanihusu mimi vile mkuu,kweli kabisa kina mjumbe alikuwa kwenye foleni tukawa tunachekeana huku moyoni nikichekelea kuwa hapo nishapata kura kumbe,ngoja nibaki kuvunjika mbavu mkuu.[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Hahahaha Hahahaha tatizo ulihama upinzani wakakushtukia tena wanaamini vijana wote wapo upinzani
 
....

FUNZO NILILOLIPATA
1. Katika kugombea kitu Cha kwanza ni MTAJI WA FEDHA KWA AJILI YA RUSHWA.
2. Jambo la pili ni UNAFIKI.
3. CV ni na ukweli ni Jambo la ziada tu.
....
Na cha nne ni uchawi hasa ukiwa CCM.
 
Fanya yote ila kama hauna ruzuku basi kura utasikilizia bombani!
 
Back
Top Bottom