Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

siku nyingine hakikisha mkeo ni mmoja wa wajumbe πŸ˜€
 
Hahaaaaa,Kama inanihusu mimi vile mkuu,kweli kabisa kina mjumbe alikuwa kwenye foleni tukawa tunachekeana huku moyoni nikichekelea kuwa hapo nishapata kura kumbe,ngoja nibaki kuvunjika mbavu mkuu.😁😁😁😁😁
Mkuu wewe ulifaa haswa kuwa diwani.
 
Wajumbe wasingekupa kura kwa vile hata wewe mwenyewe hukujipa kura yako mwenyewe ndio maana ukapata sifuri.
 
Mkuu pole hiyo ndio CCM,yanasemwa kila siku CCM ina wenyewe.

Kumbuka pia mkono mtupu huwa haulambwi mkuu.Vijana wao wanasema bila pesa hupati mchumba.
 
Mkuu,ukiwa mgombea lakini si mjumbe wa mkutano mkuu,huruhusiwi kupiga kura.Kwa mfano,katika wagombea wote 8 tuliokuwepo,ni wagombea wawili tu ndiyo walikuwa wapiga kura na wakajipigia,ndiyo maana utaona,yule aliyepata kura 23 na alikuwa mjumbe wakati yule aliyepata kura 22 hakuwa mjumbe ambapo huyu naye angekuwa mjumbe angejipigia kura na kupata 23 na kuwa sawa na mwenzake,lakini pia yule aliyepata 1 naye alikuwa mjumbe na hiyo ndiyo ilikuwa kura yake,naye naamini asingekuwa mjumbe,basi angepata sifuri Kama sisi.
 
Mkuu pole hiyo ndio CCM,yanasemwa kila siku CCM ina wenyewe.

Kumbuka pia mkono mtupu huwa haulambwi mkuu.Vijana wao wanasema bila pesa hupati mchumba.
Ahsante Sana mkuu, ulichosema ndicho nilichojifunza.
 
Mchakato wa kupata wagombea udiwani, ilikuwa muhimu isimamiwe na chama hata ngazi ya mkoa. Pia ni wakati sheria zetu kuubadikilishwa ili anagalau kuongeza sifa za mgombea, kuwa hata na elimu ya form four.........Lkn bila hivo changamoto bado zitakuwa kubwa kule halmashaur, kwa sababu madiwan wengi ni stardand 7 & 4, hivo kushindwa kuhoji kikamilifu matumiz na makusanyo ya halmashaur. Mfano ukisoma taarifa ya CAG kuhusu LGAs ni ufisadi tu, ambao unachangiwa na mabalaza mabovu ya madiwan. Hizi nafasi zinahijat angalau watu wenyew uelewa wa mambo, lkn kwa bahat mbaya zimehodhiwa na wazee fulani huko vijijini ambao mchango wao sio effective kwa maendeleo ya halmashaur mbali mbali !
 
Mkuu umenena vema Sana,basi hayo ndiyo yalinisukuma kutia Nia,nawatu niliwaeleza umuhimu wa mgombea kuwa na elimu na uelewa wa Mambo mengi utakaomboost kujenga hoja za nguvu na ushawishi lakini nikaambulia hiyo.
 
Bora wewe mkuu, wa kuonewa huruma ni Master J..yeye wajumbe walimwambia "We njoo tu kaka, kila kitu tayari huku nyoa na rasta kabisa" kinachosikitisha kakosa vyote, ubunge na rasta. Bila shaka umepata funzo kwanin mjumbe hauawi, hawauawi kwa sababu wajumbe ndo' wauaji
 
Rushwa ipo kila sehemu sio CCM tu, ipo kila chama na karibia kila taasisi. Rushwa ni tabia ya mtu sio taasisi

Huko kwengine ni shule ya msingi na chekechea , Kwa CCM ni University ya rushwa , huko watu huchukua ma degree na phds katika rushwa na roho mbaya
 
Bora wewe mkuu, wa kuonewa huruma ni Master J..yeye wajumbe walimwambia "We njoo tu kaka, kila kitu tayari huku nyoa na rasta kabisa" kinachosikitisha kakosa vyote, ubunge na rasta. Bila shaka umepata funzo kwanin mjumbe hauawi, hawauawi kwa sababu wajumbe ndo' wauaji
Kwakweli ni noma Sana.
 
Back
Top Bottom