11 January 2022
EXCLUSIVE THE BIG AJENDA USIKU WA LEO NA ALIYEKUWA MGOMBEA WA JIMBO LA KAWE, FURAHA DOMINICK.
Baada ya ukimya wa kipindi kirefu ajitokeza kwa mahojiano ya kina.
Furaha Dominic, mkemia na mbobevu wa elimu ya mazingira kwa fani alizosomea azungumzia pande mbili za uncle wake John Pombe Magufuli. Mjomba John Pombe Magufuli kuwaamini rafiki na watu wake wa karibu na hivyo wakati mwingine kutokana na imani hiyo alishauriwa vibaya na kupelekea watu kuumizwa bila kujua, na sasa 'wanamsaliti' kwa wazi Magufuli na sera zake.
Pia aliyoyaona ndani ya makundi yaliyopo ndani ya CCM kuelekea uteuzi wa kuchagua wagombea wa ubunge jijini Dar es Salaam hususan jimbo la uchaguzi la Kawe lililopo jijini Dar es Salaam. Furaha Dominick aliwahi kukamatwa tarehe 26 June kabla ya uchaguzi 2020 na kuwekwa ndani wakati wa utawala wa awamu ya 5.
Furaha Dominick visheni yake na matamanio ya CCM iende vipi na matamanio ya wananchi ... n.k n.k mengi sana.
Source: Star TV Habar
Kwanini alitaka kugombea ubunge huku akitumia mgongo wa jina la mjomba wake? Alifikiri mjomba wake angempendelea kwa kuwa ni mpwa wake? Kwanini anasema hadharani sasa hivi akisemea mambo ya kiutawala kinyume na utunzaji siri alizowahi kuziskia?
Ahojiwe pia ili aseme hadharani kuhusu kwanini JPM alipougua kwa karibu wiki mbili wananchi hawakutangaziwa mpaka alipofariki?
Ilikuwaje alikuwa anashiriki vikao vya kiongozi wa nchi na kusikiliza mazungumzo ya siri yaliyoletwa kwa raisi?
Ni akina viongozi waliokuwa wanampelekea rais taarifa za majungu na uchonganishi?
Kwanini anamwita askofu Gwajima ni muongo hadharani wakati na yeye akiwa na mgongano wa maslahi kuutaka ubunge wa Kawe?
Je, anafikiri yeye bado ni chaguo la wana Kawe kwa kipindi hiki kama ilivyokuwa enzi za JPM anayemsemea vibaya kwa sasa?
Alishaomba ushauri kutoka familia ya hayati JPM kuyasema hayo aliyotamka hadharani wakati akijua hivyo amevunja sheria?
Anatambua kwamba ili Kawe iweze kufikia maendeleo inayoyatamani kuyafikia kupitia wananchi wenyewe kwa uwekezaji wao au miradi ya serikali nisharti pawepo na ushirikiano kutoka kwa raisi, maraisi wastaafu maana wengi wana makazi huko na jeshi la wananchi kwa upande mwingine maana kambi zote kuu ziko huko?
Anatambua kwamba katika mahojiano anayoyafanya sasa hivi kwenye kituo cha runinga na kutoa matamshi tata kuhusu JPM anafufua maumivu waliyoyapata baada ya kifo chake?
Malengo yake kwa ajili ya jimbo la Kawe ambayo alikuwa anayatamani kufanyika angeyafanya kwa kutumia rasirimali fedha za kawake au kupitia mpango kazi wa serikali?